Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Mei 18, 2026 ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha maandalizi ya ushiriki wa Mkutano wa Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA) unaofanyika jijini Kigali, Rwanda kuanzia Mei 18-21, 2026.
Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Kigali na kuhudhuriwa na Waziri wa Fedha, Khamis Omar, Naibu Waziri wa Maji na Madini wa Zanzibar, Seif Pandu, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Felchesmi Mramba pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja wataalamu kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC).

Mkutano wa NEISA unawakutanisha viongozi wa serikali, wataalamu wa sekta ya nishati, wawekezaji na wadau mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika na duniani kwa lengo la kujadili ubunifu, uwekezaji na matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.


More Stories
CRDB Foundation,Zuchu wazindua jukwaa la “Zuchu – IMBEJU Masterclass
Hatifungani ya kwanza yazinduliwa iTrust
Ofisi ya Msajili wa Hazina yafanya mazungumzo na Balozi wa China