


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo akiwa Ikulu jijini Dodoma amekutana na nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea F.C. na Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba, pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.
Mkutano huo unaangaliwa kama sehemu ya kuimarisha diplomasia ya michezo (sports diplomacy), ambapo ushirikiano kati ya serikali na mastaa wa kimataifa unatumika kukuza sekta ya michezo kama kichocheo cha ajira, uwekezaji na utalii wa michezo nchini.

More Stories
Washindi ‘kila muamala bao la ushindi’ waendelea kupeta
TMA yaeleza faida taarifa hali ya hewa
Wananchi wapata elimu ubora,usalama na bidhaa