January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Bashiru aongoza mapokezi ya Mgombea Urais Dkt.Magufuli visiwani Zanzibar

Na Penina Malundo,TimesMajira,Online

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameongoza mapokezi ya kumpokea mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwasalimia viongozi mbalimbali pamoja na Wanachama wa CCM mara baada ya kuwasili Kisiwani Zanzibar wakati akitokea Tunduma mkoani Songwe

Mapokezi hayo, yamefanyika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar leo tarehe 02 Oktoba, 2020 ambapo Dkt. Magufuli ameeleza kwa ufupi,

“Leo nimeingia hapa Zanzibar, nimeingia Zanzibar kwa ajili ya kuja kufanya kampeni, kwa wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi.”

Mgombea wa Urais wa CCM,Dkt. Magufuli anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa kampeni kesho tarehe 03 Oktoba, 2020 katika viwanja vya Mnazi mmoja Mkoa wa Mjini.

Aidha Dkt.Magufuli anatarajia kufanya mkutano wa kampeni katika viwanja vya mnazi mmoja kesho ambapo atapata fursa ya kuonyesha maono yake ya ustawi wa Tanzania,Maisha ya Watu pamoja na namna atakavyoongoza ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.

Ambapo ratiba ya mkutano huo utahudhuriwa na wasanii Mbalimbali ambao ni mkada wa chama hicho na kufatiwa na maelezo yake juu ya ilani yao ya Uchaguzi inavyosema katika kipindi cha miaka mitano ijayo.