Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Mohammed (DIMW8A) amejumuika katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa Mjini Mohammed Ibrahim Hassanali (Raza lee).
Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 16 Machi, 2026 katika Ukumbi wa St. Beach Villa Kibweni – Zanzibar, Mkoa wa Magharibi Unguja, iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Madiwani wote wa Baraza la Manispaa Mjini.

Dkt. Dimwa amewaomba Madiwani kuwa na upendo, umoja na mshikamano, kuendelea kuwashajihisha wanachama na kuendelea na uingizaji wa wanachama wepya pamoja na kuzitetea hoja za Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kwa kumalizia Hotuba yake Dkt. Dimwa amewata Madiwani wote kuwa na wajib wa,
- Kukitetea Chama chake.
- Kuitetea Serikali yake.
- Kuwatetea wananchi wake waliomchagua.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Baraza la Manispaa Mjini Ndg. Mohammed Ibrahim Hassanali (Raza lee) amemshukuru Dkt. Dimwa kwa uzalendo anaonesha katika utendaji na usimamizi bora wa kazi za Chama cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar, pia amewasisitiza Madiwani wa Baraza la Manispaa Mjini kuwa umoja na ushirikiano ndio unaodumisha uletaji wa maendeleo.




More Stories
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini