March 12, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Msichana Initiative yazindua mradi wa Renewed Women Voices and Leadership Tanzania

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

SHIRIKA la Msichana Initiative limezindua   rasmi mradi wa Renewed Women Voices and Leadership Tanzania (RWVL-T) na kuwakutanisha wanawake viongozi vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo Ruvuma, Kigoma, Kagera, Tanga, Arusha, Dodoma, Shinyanga, Katavi, Mbeya na mingine mingi.

Mradi huu unalenga kuimarisha sauti, uongozi na ushiriki wa wanawake katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kisera. Pamoja tunajenga mtandao imara wa wanawake viongozi vijana kutoka mikoa yote Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo Mkurugenzi  wa Shirika hilo,Consolata Chikoti amesema kuwa changamoto ya upatikanaji wa rasilimali naufadhili kwa mashirika ya wanawake ni changamoto sugu,si tu Tanzania bali duniani kote.

Amesema tafiti nyingi zinaonyesha kuwa mashirika ya wanawake hupokea sehemu ndogo sana ya fedha za maendeleo, licha ya kuwa mstari wa mbele katika kushughulikia masuala muhimu kama haki za wanawake, afya, elimu, usawa wa kijinsia na maendeleo ya jamii.

Amesema  lengo la kusaidia wanawake – hususan vijana wanawake kuimarisha uwezo wao wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii na katika uongozi.

Amesema mashirika ya wanawake mara nyingi ndiyo yanayofanya kazi karibu zaidi na jamii, yakifikia makundi yaliyo pembezoni na kutoa suluhisho bunifu kwa changamoto zinazokabili wanawake na wasichana.

”Mara nyingi kazi hii kubwa hufanywa kwa rasilimali chache sana.ndiyo maana miradi kama huu ni muhimu sana. Kwa kutoa rasilimali, kujenga uwezo, na kuimarisha uongozi, tunasaidia si tu mashirika ya wanawake, bali pia tunachangia kujenga jamii yenye usawa zaidi, haki zaidi, na maendeleo endelevu.

”Kaulimbiu ya “Give to Gain” ina maana kubwa sana katika muktadha huu unapowekeza kwa wanawake, tunapata jamii yenye afya bora, uchumi imara zaidi, na demokrasia jumuishi zaidi,”amesema Chikoti.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mradi,Navina Mtabazi,amesema mradi huo ni  wa kujengea uwezo viongozi wanawake ambao ni vijana pamoja na upazaji sauti zaidi kwenye masuala ya uongozi na uamuzi.

Amesema  lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwambawanawake walioanzisha mashirika wanauwezo wa kuendeleza mashirika yao na mifumo yao kwa usahihi.

‘Kuwajengea wao kiuongozi kufanya maamuzi ambayo ni sahihi na yenye ubora kwenye mashirika yao.

”Mradi  huu unalengo la kutengeneza movement kwa wanawake vijana viongozi kuweza kupaza sauti kwa pamoja katika masuala mbalimbali hususan masuala ya kijinsia,”amesisitiza