March 10, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mkuu apongeza ujenzi bora wa uwanja wa ndege Sumbawanga

Na Israel Mwaisaka, Online Majira Rukwa

‎Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Rukwa kwa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Sumbawanga kwa ubora.

‎Amesema hayo  leo Marchi 8,2026 alipokagua maendeleo ya ujenzi huo na kusisitiza kuwa kiwanja hicho kimejengwa kwa viwango vya kisasa.

‎” Hongereni wana Rukwa kwa kupata kiwanja cha ndege cha kisasa kitakachochochea fursa nyingi za kiuchumi”, amesema Dkt. Nchemba.

‎Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema ujenzi wa kiwanja cha ndege hicho unaotekelezwa na mkandarasi M/s Beijing Construction  Engineering Group Co Ltd kutoka China umefikia asilimia 96 na utakamilika ifikapo April mosi mwaka huu.

‎Nae Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema wako tayari kukipokea kiwanja hicho mapema mwezi ujao ili kuanza kutoa huduma za ndege mkoani humo.

‎Kiwanja cha ndege cha Sumbawanga ambacho kilijengwa mwaka 1945 na kukarabatiwa mwaka 1985 kimefanyiwa uboreshaji mkubwa na wa kisasa utakaowezesha ndege za saizi ya kati kutumia kiwanja hicho ambapo zaidi ya shilingi bilioni 60 zimetumika