March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani

‎Na Israel Mwaisaka, Nkasi

‎Kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani jumuia ya kikristo Tanzania (CCT) idara ya Wanawake imefanya kongamano kubwa ambalo limewakumbusha wajibu wao na kutambua haki zao ikiwa ni pamoja na kumtanguliza Mungu kwa Kila jambo.

‎Akitoa mahubiri kwenye kongamano hilo lililofanyika katika kanisa la Anglikana mjini Namanyere  mhubiri Debora Kaguo alidai kuwa Mwanamke ndiyo nguzo kuu katika malezi ya familia hivyo anatakiwa kuwa ni Mtu anayejitambua na kujua anachokifanya.

‎Amesema kuwa ndoa kwa kiasi kikubwa inajengwa na Mwanamke na kuwa ni jukumu la Mwanamke kumlinda Mumewe lakini si kwa kukagua simu akiwa amelala au kumfuata Kila aendako na kwenda kuanzisha ugomvi na Wanawake wengine Wenye mahusiano na Mume wako Bali ni kumhudumia vyema na kumuombea mbele ya Mwenyezi Mungu

‎Mhubiri Kaguo amesema kuwa kwa Sasa ndoa nyingi ni za moto hivyo ni muhimu kwa Sasa wakautumia muda mwingi kuzirekebisha ndoa zao badala ya kuutumia muda mwingi kuzungumza mambo yasiyokuwa na msingi Wala tija kwao

‎Mgeni rasmi katika kongamano hilo ambaye ni afisa elimu msingi Eliud Njogela ambaye aliwakilishwa na Noel Kiombo aliwakumbusha Wanawake kuendelea kulinda heshima ya Mwanamke kwa kuwa wanyenyekevu na wenye kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao