Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online, Mbeya
WABUNGE wawili Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambae ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge pamoja na Mbunge Jimbo la Uyole Dkt. Tulia Ackson wakutana kutatua changamoto kwenye barabara inayounganisha majimbo hayo kwa lengo la kuondoa adha wanazo kumbana nazo wananchi.
Akieleza kwa undani Dkt. Tulia amemweleza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya ambae ni Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini Patrick Mwalunenge kuona namna ya kushirikiana na serikali kukamilisha ujenzi wa kiwango cha zege unaofanywa na wadau kwa kushirikiana na wananchi ili kuweza kuunganisha majimbo hayo mawili.

Dkt.Tulia amesema kuwa pamoja na kufunguliwa kwa barabara ya pepline haraka iwezekanavyo ili kurahisisha shughuli za kijamii ndani ya kata hizi mbili kata ya Mwakibete pamoja na kata ya Iyela zinazo unganisha majimbo haya mawili.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM ambae ni Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini Patrick Mwalunenge ameahidi kuchangia milioni.10 ili kukamilishwa haraka kwa hii barabara kwa kiwango cha zege ikiwa ni pamoja na kufanya mkutanao na wana Iyela ili kuchangia maendeleo hayo yaliyo anza kufanywa na wana Bombambili kutoka kata ya Mwakibete.
Ameeleza kuwa hiyo ni mara yake ya kwanza kufika kwenye eneo hilo linalo unganisha majimbo hayo mawili na kufurahishwa kwa namna ambavyo wadau na wananchi wameungana kuleta maendeleo kabla ya serikali kuwafikia.
Mmoja wa wananchi Kata ya Mwakibete, Nuru Jeremeh amesema kuwa kitendo cha wabunge hao kuungana pamoja kitaleta tija ya pamoja ya kuleta maendeleo katika jimbo la Mbeya mjini na Uyole.


More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi