Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dodoma
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kupokea masikitiko taarifa ya kifo cha Baba Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar-es- Salaam,kilichotokea usiku wa Februari 19,2026,katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar.
Katika taarifa iliotolewa Februari 20,2026 na Katibu NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi,imesema Chama Cha Mapinduzi,kinatambua na kithamini mchango mkubwa wa mwadhama Kadinali Pengo,katika kulihudumia Kanisa Katoliki na Taifa kwa ujumla kupitia uongozi wake wa kiroho, maadili na huduma za kijamii.
“Katika kipindi hiki, CCM kinaungana na Kanisa Katoliki Tanzania, familia, waumini na Watanzania wote kuomboleza msiba huu mkubwa wa kuondokewa na kiongozi wetu wa kiroho, tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, mahali pema peponi,”imesema sehemu ya taarifa hiyo.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina