Na mwandishi wetu Timesmajira Online-Bukoba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Kido,amesema suala la ulinzi na usalama litakuwa kipaumbele namba moja katika uongozi wake kwa kushrikiana na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo .
Kanali Kido, amesema hayo mara tu baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajath Fatma Mwassa na kusema kuwa uteuzi wake ni heshima kubwa na dhamana nzito,atahakikisha anatekeleza maelekezo yote ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hususan yale ya kuimarisha uwajibikaji na kusimamia maendeleo ya wananchi.

“Nitasimamia miradi yote ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na itakayopangwa ili thamani yake iendane na fedha iliyotolewa na serikali,”amesema Kanali Kido.
Amesema atahakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati ili huduma zipatikane kwa wananchi kama yalivyo matarajio yao.
Hata hivyo Kanal Kido amehaidi kuendeleza pale alipoishia mtangulizi wake na kuongeza nguvu katika maeneo yanayohitaji maboresho zaidi.
Awali aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Hajat Fatma Mwassa,amesema Mkoa huo unakabiliwa na tatizo la uhamiaji haramu.
Hajati Mwassa,amesema kipindi cha Novemba 2024 hadi Novemba 2025 zaidi ya wahamiaji haramu 17,200 walikamatwa mkoani kagera walioingia kinyume cha sheria na kurejeshwa kwao.
Hata hivyo amesema Mkoa umeweka mikakati ya kutoa ajira kwa vijana ambapo kila wilaya itatakiwa kutengeneza ajira 2000 kila mwaka za vijana.



More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina