March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt Maghembe akutana na Balozi wa Cuba nchini,kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dkt. Ngwaru Maghembe,amefanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini Tanzania,Yordenis Despaigne Vera, katika ofisi ndogo za Wizara hiyo , jijini Dar-es-Salaam.

Mazungumzo hayo yamefanyika Februari  10,2026,yakilenga kujadiliana namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Cuba.

Ikumbukwe kuwa,Tanzania na Cuba zimekuwa na uhusiano wa karibu na kindugu zaidi ya miongo sita iliyopita ambapo nchi hizo mbili zilianzisha ushirikiano wa kidiplomasia mwaka 1962.

 Uhusiano huo  umejengwa tangu enzi za kupigania uhuru ambapo viongozi waasisi wa mataifa hayo  Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Hayati Fidel Castro wa Cuba, ambao walijenga msingi wa uhusiano, usawa na maendeleo ya pamoja. 

Kwa pamoja viongozi hao, wamejadiliana namna bora ya kuendeleza ushirikiano wa uwili na kimataifa kwa maslahi ya pande zote mbili.