Na Zena Mohamed,TimesMajiraOnline,Dodoma
BARAZA Kuu la Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa limetia tamko la pongezi kwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt.Hussein Ali Hassan Mwinyi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu 2025.
Akisoma tamko la Baraza hilo jijini hapa leo Januari 17,2025 Katibu Mkuu Umoja wa Wazazi wa CCM Taifa Ali Hapi amesema kuwa wanawapongeza viongozi hao kwa kuzingatia imani kubwa ambayo wamepewa Dkt.Samia na Dkt.Mwinyi na Wananchi wa Tanzania ambao ndiyo msingi wa Mamlaka ya Nchi na kumchagua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kishindo pia.

“Sisi wajumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa kwa kuzingatia Ibara ya 5 ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la 2025 inayoeleza malengo na Madhumuni ya CCM na Ibara ya 5 (1)inayofafanua malengo mahsusi kuwa ninkushonda katika uchaguzi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande mmoja na Zanzibar kwa Upande wa Pili na
“Ibara ya 125(1)-(c) ya Katiba hii inayoonesha Jumuiya zinazoongozwa na CCM na kwa umahsusi ikiitajika Jumuiya ya Wazazi na kwa kuzingatia Kanuni ya Umoja wa Wazazi Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2022 Uk IV-V(1-8)inayofafanua kwa kina wajibu na Majukumu ya Jumuiya ya Wazazi,”amesema Hapi.
Hapi amesema wao kama wajumbe wa Baraza Kuu la Wazazi wa CCM Taifa Chombo cha Kikatiba na Kikanuni wanaopewa mamlaka ya usimamizi wa shughuli za umoja wa Wazazi kutoka kwenye Kanuni ya Wazazi Ibara 88(1-16)wanatoa tamko kwa kauli moja kumpongeza Dkt.Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu 2025.
“Jumuiya ya Wazazi itaendelea kumuunga mkono yeye na Serikali ya CCM katika utekelezaji wa majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu,”amesema Hapi.

Aidha Baraza hilo linampongeza Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vilevile amesema kwa Kauli moja Baraza Kuu hilo linampongeza Dkt.Mwinyi kwa ushindi katika Uchaguzi Mkuu 2025 kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambapo limesema litaendelea kumuunga mkono yeye na serikali ya CCM katika kuwaletea maendeleo endelevu wananchi wa Zanzibar.
Pia Baraza hilo limempongeza Dkt.Mwigulu Nchemba kwa kuaminiwa na Rais kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Uteuzi wake ni kielelezo cha imani kubwa ya Mhe.Rais kwake,vilevile linampongeza Mhe.Hemed Suleiman Abdulla(MBW)kwa kuaminiwa na Mhe.Rais wa Zanzibar na kumteua kwa awamu ya pili kuwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,uteuzi wake ni uthibitisho wa imani aliyonayo Mhe.Rais wa Zanzibar kwake,”amesema.

Pamoja na hayo Baraza hilo limesema linaunga mkono jitihada za serikali za kuhimiza amani mshikamano na umoja wa Taifa ili kuleta maendeleo endelevu wananchi.
“Jumuiya itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kukijenga chama na kuwa sauti ya kuzisemea na kuzifafanua kazi nzuri zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,”amesema Hapi.




More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi