Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Wilbert Yona(34), mfanyakazi katika kiwanda cha Ziwa Steel na mkazi wa Kata ya Ihayabuyaga, wilayani Magu mkoani Mwanza,anadaiwa kumuua mpenzi wake aitwaye Marietha Kalafala(33),pia ni mfanyakazi wa kiwanda hicho na mkazi wa Mwabuyi, kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kisha na yeye kujinyonga.
Akizungumza tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbord Mutafungwa,amesema tukio la vifo vya watu wawili vilivyotokea tarehe tofauti Desemba 27 na 28,2025.
Ambapo tukio la mauaji ya Marietha Kalafala yaliripotiwa Desemba 27,2025, majira ya 2 na dakika 15 usiku, katika Kitongoji cha Mwabuyi, Kata ya Nyanguge, Wilaya ya Magu,ambaye
aliuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni, mgongoni na kwenye paji la uso kisha wili wake kutupwa kwenye shamba la mahindi.
Mutafungwa amesema,baada ya ufuatiliaji ndipo Desemba 28,2025, majira ya 3.00 asubuhi, katika nyumba ya
kulala wageni itwayo Wema, iliyopo Kata ya Nyanguge Wilaya ya Magu, Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa mmiliki wa nyumba hiyo kuwa kuna mteja wao amejiua kwa
kujinyonga kwenye chumba alichokuwa amekodi.
“Baada ya Askari Wetu kufika
kwenye nyumba hiyo mwili wa mtu huyo ulitambuliwa kuwa ni Wilbert Yona,
aliyekuwa anatafutwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Marietha,”amesema Mutafungwa.
Amesema,miili ya marehemu imehifadhiwa katika kituo cha afya Lugeye, wilayani Magu, kwa
ajili ya uchunguzi wa kitaalamu na utakapokamilika miili itakabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.
Hata hivyo ametaja chanzo cha matukio haya ni wivu wa kimapenzi kwani
inadaiwa Yona ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa akimtuhumu Marietha(marehemu) kuwa
na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.
Sanjari na hayo ametoa wito kwa wananchi hususani wapenzi na wana ndoa kuacha kujichukulia sheria mkononi wanapopata migogoro ya kimapenzi au ya kifamilia.
Na badala yake watafute msaada wa ushauri kupitia watu wanaowaamini, ustawi wa jamii, viongozi wa dini au vituo vya huduma ya kisaikolojia pale wanapopitia migogoro ya
kifamilia.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi