Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KATIBu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano,Mary Maganga, amesema Wakala wa Usalama na Afya Mahali pakazi (OSHA) ni taasisi yenye umuhimu na nafasi kubwa Katika kuwezesha shughuli za uzalishaji kufanyika kwa tija.
Maganga ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha tano jijini Dodoma, ambapo amewasisitiza watumishi wa OSHO kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kadri ya kanuni za utumishi wa umma pamoja na kuimarisha ushirikiano baina yao.
“Niwatake kufanya kazi kwa weledi,tumekuwa tukiamini kwamba wito unahusiana na shughuli za viongozi wa dini pekee lakini tunasahau kwamba hata kazi zetu ni wito,kwani majukumu yetu ni lazima tufanye kwa ajili ya watu ambao wanategemea huduma zetu,” ameeleza Maganga
Awali Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda, amesema kikao hicho kinalenga kutathmini utendaji wa taasisi hiyo kwa kutazama kipindi kilichopita na kilichopo ili kupata mustakabali wa maendeleo katika kipindi kijacho.
“Kikao hiki pamoja na kutathmini utendaji wa yaasisi kwa mwaka wa fedha 2024/2025,kinalenga kuangalia mwenendo wa utendaji wetu katika miezi mitano iliopita mwaka huu wa fedha (2025/2026 hususani katika kipindi hiki tunapoelekea kuandaa bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027,” amesema Mwenda.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE),Rugemalila Rutatina, ameipongeza OSHA kwa kuwa na utaratibu mazuri wa ushirikishwaji watumishi wote pasipo ubaguzi katika kufanya maamuzi ya masuala muhimu yanayohusu utendaji wa Taasisi hiyo.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi