*Ni kupitia programu ya Kafiti na Bodaboda
*Kuwezesha vijana wa kata 19 kujiajiri na kuimarisha uchumi
*Asema mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake za siku 100 za mwanzo
Judith Ferdinand,Mwanza
Katika kutekeleza ahadi zake za siku 100 za mwanzo, Mbunge wa Jimbo la Ilemela,Kafiti Kafiti, amejipanga kutoa bodaboda 100 kwa vijana wa Kata 19 za Jimbo hilo, hatua ambayo ni fursa muhimu ya kuwawezesha kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.
Pamoja na kukutana na vijana na wanawake ambao wamehitimu mafunzo ya stadi katika fani mbalimbali yaliotolewa na Chuo cha Ufundi Stadi(VETA) Mwanza,ili kuwezesha vikundi vyao kusajiliwa na kupata mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri.

Kafiti amezungumza hayo Desemba 17,2025, mara baada ya kufungua mahafali ya mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na wanawake wa Wilaya ya Ilemela na Nyamagana yaliofanyika kupitia programu ya Wanawake na Samia pamoja na mradi wa Vijana, Elimu, Malezi na Ajira(VEMA) unaotekelezwa na shirika la Plan International yaliofanyika VETA.
Ambapo amesema,yupo tayari kuona vijana wanainuka kwani anaamini wakiwasaidia wakaweza kujiajiri itasaidia kujikwamua kiuchumi binafsi na taifa kwa ujumla.
Amesema wakati wa kampeni moja ya ahadi ambayo aliahidi kuitekeleza ndani ya siku 100 za mwanzo za uongozi wake ni kutoa bodaboda 100 kwa vijana wa kata 19 p jimboni Ilemela kwa maana kila kata itapata bodaboda 5.
“Programu hiyo inaitwa Kafiti na Bodaboda,na sasa hivi tunamalizia kuwasajili na Mungu akijalia Desemba 20,2025 tutakabidhi bodaboda hizo kwa vijana.Nitahakikisha kila bodaboda jimboni Ilemela anapata leseni pamoja na elimu ya kuendesha chombo hicho kwani kundi hili limeajiri vijana zaidi ya 10,000,”amesema Kafiti.
Pia amesema,wataendelea kuhakikisha vijana wenye elimu tofauti wanaweza kujikwamua kiuchumi ambapo kuna baadhi yao kama Mbunge atawashika mkono katika eneo la kuajiriwa na wengi katika kujiajiri kwa kuwapa mafunzo na ujuzi huku jambo kubwa atakalolifanya ni kuwapa mitaji pamoja na kuwezesha wajasiriamali wadogo.
“Kupitia programu hizo za Wanawake na Samia na mradi wa VEMA,i nimeisha ongea na uongozi wa VETA,Desemba 29,2025 tutakutana hapa na wahitumu hao tukiwa na Maofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Ilemela ili kuweza kuwaunganisha katika vikundi,kuwasajili kutoa elimu ya namna ya kuingia katika mfumo ili tuweze kuwapatia hiyo mikopo ya asilimia 10 na kuweza kujiajiri,”amesema Kafiti.

Kwa upande wake Mratibu wa Wanawake na Samia wa Wilaya ya Ilemela,Zuhura Salaam,amesema mafunzo hayo yalianza Septemba 2025 chini ya ufadhili wa Rais Samia Suluhu Hassan yakiwa na lengo la kusaidia wanawake kupata ujuzi wa fani mbalimbali nchini kupitia vyuo vya ufundi stadi(VETA).
Zuhura amesema,ambapo Mkoa wa Mwanza ulianza na wanawake 2214 kwa awamu mbili huku waliofanikiwa kuhitimu mafunzo hayo katika kozi 15 ni wanawake 1912,waliokatisha mafunzo ni 300 huku aliyefariki akiwa mmoja.
“Awamu ya tatu ya mafunzo hayo inatanza Januari 2026 ikitarajia kushirikisha wanawake 515.Tunaomba tupate mikopo ya asilimia 10 kwani elimu tayari tumeisha pata,ofisi ya Wanawake na Samia kwa Mkoa wa Mwanza pamoja na kupata mitaji wezeshi kupitia sekta binafsi na Serikali,”amesema Zuhura.
Huku akibaisha changamoto zilizowakabili baadhi ya wanawake na kushindwa kuendelea na mafunzo ni pamoja na kuzuiliwa na wenza wao kwa sababu zao binafsi.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako