Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
WASHIRIKI watano wa droo ya kwanza ya kampeni ya ‘Chanja kijanja, dili ndio hili’ wamejishindia zawadi ya shilingi 100,000 kila mmoja.
Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim, Silas Matoi, aliwatangaza washindi hao mwishoni mwa wiki, huku akisema kuwa washindi hai watakuwa wakitangazwa kila wiki mpaka mwisho wa kampeni hiyo.
“Kila wiki, washindi watatangazwa, na kila mwezi washindi 10 watashinda sh. 200,000. Vilevile washindi wa droo kuu watapokea zawadi kubwa za sh. milioni 5, milioni10, na mshindi mkuu sh. milioni 15,” amesema Matoi.
Benedict Mwinula, Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali, pamoja na Rodgers Biteko, Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika droo hiyo.
Kampeni ya Chanja Kijanja inalenga kuwapa wateja wa Exim fursa ya kushinda kila wanapotumia kadi za benki hiyo kulipia bidhaa au huduma.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako