Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Wenyeviti wa mitaa ya nane ya Kata ya Pasiansi wameombwa kusaidiana mabalozi kutengeneza kamati za ulinzi shirikishi ili kuimarisha ulinzi wa kila mtaa na kuchochea amani ya taifa.
Wito huo umetolewa Desemba 11,2025 na Diwani wa Kata ya Pasiansi, Regina Lubala,katika kikao chake cha kwanza na makundi mbalimbali kwa ajili ya kutoa muelekeo wa miaka mitano ya uongozi wake katika Kata hiyo,ambapo amesisitiza kila mmoja kuwa mlinzi wa mahali anapoishi.

“Hakuna maendeleo bila ya kuwa na usalama,hakuna maendeleo yoyote yatakayoweza kufanyika kwenye kata yetu kama usalama wetu hautakuwa mzuri,kama ulinzi wa kata yetu hakutakuwa mzuri,”amesema Regina na kuongeza:
“Natamani sana katika kata yetu tuwe na ulinzi na usalama ili tuweze kuleta maendeleo ambayo yatatufaa na kutusaidia hapa Pasiansi,”.
Regina amewasisitiza Wenyeviti wa mitaa hiyo na Mabalozi kila mmoja atazame kwa umakini ni namna gani katika mtaa au eneo analoliongonza Kuna kuwa na ulinzi na usalama.
Pia amewaomba Mabalozi kuhakikisha na kutambua kila mmoja anayeingia katika mtaa au eneo lake analoongoza kwa kuhakikisha wanafahamj au kutambua mwananchi huyo anatoka wapi,je amehamia au amekuja kusalimia na kuondoka.
“Muwatambue wananchi wanaotoka na kuingia katika mitaa yetu,zamani sana sisi wakati tuna kua,mgeni anapoingia ilikuwa lazima akaripoti kwa Balozi.Lakini siku hizi imekuwa ni holela tu mgeni anaingia anakaa anavyotaka na kuondoka,”amesema Regina na kuongeza:
“Mbaya zaidi unakuta mtu anahamia mtaani ajulikani na Balozi wala Mwenyekiti anaishi tu bila shida kwa sababu tunajua watanzania ‘hatunaga’ matatizo anaishi kwa amani yake,halafu hatujui kule alipotoka alikuwa na kitu gani ambacho kinaendelea,”.
Sanjari na hayo,Regina amewahimiza wenyeviti na jamii kwa ujumla kuwasaidia vijana namna gani ya kuishi,maadili na mienendo mizuri ili Kata hiyo iwe nzuri yenye kuaminika na salama.
“Usimwangalie mtoto ukasema ni mtoto wa fulani au siyo wa kwangu,msaidie ata kama siyo mtoto wako ili aje atufae, maana akiwa mtukutu katika mtaa hata tesa familia yake tu bali ata wewe utaingia katika kuteseka,”amesema Regina.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekekalezaji wa shughuli za maendeleo zilizofanyika kipindi ambacho Kata hiyo haikuwa na Diwani,Mtendaji wa Kata ya Pasiansi,Maarufu Mohammed,amesema,hali ya ulinzi na usalama katika kata kwa ujumla ni nzuri kiasi maana hakuna matukio ya uhalifu.
“Juhudi za kuendelea kuhamasisha uwepo wa amani ndani ya mitaa yote na kata zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwa na vikundi vya ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na polisi kata,”amesema Maarufu.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa shule ya sekondari ya wavulana Bwiru,Mhela Ngasa,ameomba wadau kuwasaidia kujenga uzio katika shule hiyo ili kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanafunzi.
Ngasa,amesema wanapata changamoto ya kuwalea na kuwalinda wanafunzi wao hasa nyakati za usiku kutokana na shule hiyo kutokuwa na uzio wala sehemu ambayo wanaweza kuwazuia ili wasiweze kutoroka.
“Tunaomba mtu atusaidie tupate mfadhili wa uzio angalau kwa kuanzia hususani maeneo ya mlimani.Kwa sababu kule milimani vijana mara nyingi wanatoroka,wanapotelea kule na mwisho wanafundishwa kuvutu bangi,”amesema Ngasa na kuongeza:
“Kwa kuwa tumeongelea suala la ulinzi na usalama,nimuombe kuna vijana uwa wanampenda kukutana kule milimani wanajifanya ni wavuvi kumbe siyo,ni wauza bangi na dawa za kulevya wanatufundishia wanafunzi wetu tabia mbaya na tunakoelekea watakuja kutusumbua sana,”.


More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina