March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kihongosi: Vijana msikubali kutumika lindeni amani

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online- Dar

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM),kimewasihi vijana kutokubali kutumika kwa maslahi ya watu wengine wasiokuwa na nia njema na nchi badala yake waelewe jukumu lao la kulinda amani na usalama wa taifa.

Akizungumza kwenye kikao kazi na viongozi mbalimbali wa CCM, Desemba 6,kijini Dar-es-Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi amesema ni vyema vijana na wananchi wote kwa ujumla wakawa wazalendo kwa kuhubiri amani na siyo kukubali kuichoma nchi au kutumika kwa maslahi ya wengine wasiokuwa na nia njema.

“Tusikubali kuingia kwenye mkumbo utakaogharimu maisha yetu, nawaomba tusiwe sehemu ya vurugu,vijana msikubali kutumika kwa yasiostahili kwani pindi yanapotokea matatizo mnabaki wenyewe na kuwapa shida wazazi,”amesema Kihongosi.

Amesema,vijana hawapaswi kubeba ajenda wasizozijua wala wasikubali kuwa biashara na kukubali kutumika kwa maslahi ya watu, akisisitiza waowashawishi kufanya vurugu wanawaita waliopata madhara yale ni mashujaa wakati wao wamejificha katika mataifa ya watu.

Kihongosi amesisitiza kuwa kila mmoja ana jukumu la kulinda amani na kuhakikisha taifa linabaki salama, kwani hakuna atakaye baki salama ikiwa taifa litachafuka.

“Usalama ni jukumu la kila mtanzania na kulinda amani ni kulinda mustakabali wa taifa” amesema Kihongosi.

Sanjari na hayo amesema, changamoto za ndani ya nchi zitatatuliwa ndani ya taifa, akibainisha kuwa Tanzania ni nchi pekee iliyosalama kati ya mataifa yote yanayolizunguka yanashida, hivyo amewataka watanzania kulinde nchi yao na wasiharibu mahali walipozaliwa.

“Tume ya uchunguzi imepewa miezi mitatu itachunguza na kuja na majibu, tuiache ifanye kazi ,mtu kabla tume haijamaliza kazi yake wameanza kuipinga unaogopa kitu gani,” amesema Kihongosi.

Pia amemesema baadhi ya watu wanatumia mitandao kuhamasisha vurugu na wengine hushabikia bila kujua madhara yake.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar-es+ salaam, Albert Chalamila amewataka watanzania kuacha ushabiki wa mambo na badala yake wajenge taifa lililo moja kwani huu si muda wa ushabiki, marumbano wala kunyoosheana vidole.

“Uchaguzi tukae pamoja kujenga ushirikano kwa mustakabari wa nchi,inawezekana kuna na taasisi ya elimu,dini au chama yenye mawazo wanaruhusiwa kuja kuzungumza na serikali ili tuweze kujenge taifa,” amesema Chalamila.