Na Mwandishi wetu,Timesmajira
IMEELEZWA kuwa waandishi wa habari ni vinara katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo chanya kufuatia kuandika taarifa za kizalendo zilizo na mizani ndani ya Taifa lao na jamii kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa halmashauri mkuu wa Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) Sheikh Khamis Mataka amesema waandishi wanawajibu mkubwa wa kutumia vema taaluma yao kwa kuandika kwa usawa katika kuuhabarisha umma.
“Vyombo vya habari ni mhimili wa nne katika mihimili muhimu ya nchi hii uandishi huo unatakiwa kufuata mabadiliko ndani ya jamii sio kuandika taarifa za uchochezi ambazo ni dhambi kubwa kwa mungu,” amesema Sheikh Mataka
Aidha Sheikh Mataka amewataka washiriki hao kuzingatia weledi wa taaluma zao lakini kuepukana na uchochezi ambao ni Miko kwa wanahabari kwa kuandika habari za upande mmoja, zisizo na uchunguzi.
Mkuu huyo amesema kwamba vyombo hivyo vina nafasi kubwa Katika kutoa taarifa zenye kusababisha taharuki na mpasuko ndani ya jamii yetu hivyo aliusia usawa, kutokuweka maslahi mbele sambamba na kuweka usahihi wa taarifa kutawafanya waandishi kuandika taarifa zao kwa weledi.

Kufuatia vurugu, maandamano Sheikh Mataka amewataka wanahabari kutumia vema kalamu zao kwa usahihi wa taarifa bila kuegemea upande mmoja ambao waweza kuwa changamoto kwa watu wengine na hasara kwa nguvu kazi ya Taifa kwa kusababisha kutumia ama kupoteza maisha.

Hata hivyo katika Semina hiyo iliyojaa usikivu wa hali ya juu na wanahabari kuuliza maswali kadha wa kadha kulingana na umuhimu mkubwa wa kuuhabarisha umma wa watanzania na Taifa kwa ujumla wake pia aliusia kuwapenda viongozi wetu ambao ndio wabeba maono wa nchi yetu.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi