November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baadhi ya wanawake walioshiriki mafunzo ya elimu ya afya ya uzazi na malezi ya mtoto wakila kiapo cha kutokiuka utaratibu wa kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kwa kipindi kisichopungua miezi sita bila kuwapa chakula chochote ,Kiapo hiki kimefanyika baada ya somo husika kutolewa kwa washiriki wote.

Wanawake Njombe washauriwa ushauri wa afya katika ukuaji wa mtoto

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Njombe

WANAWAKE mkoani Njombe wametakiwa kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu wa afya katika malezi na ukuaji wa mtoto kutoka kipindi cha kuzaliwa mpaka anapofikisha umri wa miaka mitano ili kuweza kumsaidia mama na mtoto kuwa na afya njema.

Baadhi ya wanawake wilayani wanging’ombe wakiingia ukumbini tayari kwaajili ya kupata elimu ya afya ya uzazi na malezi ya watoto iliyoandaliwa na Mradi wa USAID Tulonge afya wilayani humo.Mpigapicha Wetu

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Afya ya Mama na mtoto wa Wilaya ya Wanging’ombe Edshan Mtega wakati wa shughuli ya kina mama wenye watoto wa chini ya mwaka mmoja iliyoandaliwa na mradi wa USAID Tulonge Afya kupitia jukwaa la Naweza kwa kushirikiana na uongozi timu ya afya ya Wilaya wa Wanging’ombe.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo iliyopewa jina la “Mothers Meet Up Events” ikimaanisha “Shughuli ya Kukutana kina Mama” ambayo ilifanyika katika ya Wilaya ya Wanging’ombe wisho wa wiki hii Mratibu huyo wa Afya ya Mama na Mtoto wilayani Wanging’ombe Edshan Mtega alisisitiza kuwa malezi bora kwa mtoto chini ya miezi sita ni muhimu sana katika kuchochea afya njema kwa mtoto katika kipindi cha utotoni mpaka anapokuwa mtu mzima.

Baadhi ya wanawake walioshiriki mafunzo ya elimu ya afya ya uzazi na malezi ya mtoto wakila kiapo cha kutokiuka utaratibu wa kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kwa kipindi kisichopungua miezi sita bila kuwapa chakula chochote ,Kiapo hiki kimefanyika baada ya somo husika kutolewa kwa washiriki wote.

Mtega amesema kuwa lengo la shughuli hiyo ni kupeana uzoefu na kukumbushiana kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa malezi ya mtoto kuanzia kipindi cha kuzaliwa mpaka kufikia umri wa miaka mitano ikiwemo Mama kulala ikiwemo kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kwa kipindi miezi sita bila kumpa kitu chochote,kulala kwenye chandarua chenye dawa kila siku, matumizi ya njia za kisasa za afya ya uzazi.

“Matumizi ya njia za kisasa za afya ya uzazi ni muhimu kwani inatoa nafasi kwa mama kufanya shughuli zaidi za kiuchumi, mtoto anakuwa vizuri na vilevile wazazi uweza kuamua muda muafaka wa kupata mtoto mwingine’, amesema Mtega.

Mtega amewasisitiza pia mama anapoona dalili hatarishi kwa mtoto ni vyema akampeleka hospitali kupata matibabu sahihi na kuondokana na Imani potofu na kufikia akina mama wengine kwenda kupata tiba ya miti shamba ambayo inaweza kuhatarisha zaidi Maisha ya mtoto.

Ametoa shukrani kwa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo wilayani humo ikiwamo mradi ya Tulonge Afya unaotekelezwa kupitia ufadhili wa shirika la Marekani liitwalo USAID.Mradi wa USAID Tulonge afya unahamasisha mabadiliko ya tabia chanya ndani ya jamii ili kuiwezesha kuwa na Afya njema.

Kwa upande wake, mratibu wa shughuli za mradi wa USAID Tulonge Afya kwa mkoa wa Njombe,Edgar Mwakisu amesema kupitia Jukwaa la Naweza kina jamii kwa ujumla inapewa elimu mbalimbali juu ya ujauzito na malezi ya mtoto mpaka kufikia umri wa miaka mitano.

Ameongeza kuwa Wilaya ya Wanging’ombe ni miongoni mwa wilaya ambazo zimepewa kipaumbele katika utekelezaji wa mradi huu ikiwa ni miongoni mwa wilaya zinazotajwa kuwa na changamoto kwenye malezi ya watoto chini ya miaka mitano