March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

 Waziri wa Viwanda na Biashara afanya ziara

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga,amefanya ziara ya kutembelea ofisi ya Tume ya Ushindani(FCC), kwa lengo la kuogeza ufanisi katika ufanyaji wa majukumu mbalimbali ya kazi.

Kapinga amefanya ziara hiyo Novemba 24,2025  wakati alipotembelea  ofisi za FCC,zilizopo jijini Dar-es-Salaam,ambapo amesema,Tume hiyo inafanya kazi ya kudhibiti, kulinda walaji,  bidhaa feki  pamoja na utoajia elimu ya masuala ya kibiashara ikiwemo muunganiko wa kampuni kubwa.

Pia kuhakikisha muunganiko huo wa ushindani unaleta manufaa kwenye shughuli za kibiashara.

“Kikao cha leo kinalenga namna nzuri ya utendaji kazi ili kufikia mategemeo na matarajio ya Watanzania ambao ni walaji pamoja na kuongeza njia ya kuwafikia zaidi ili kupata mrejesho wa kazi tunazozifanya kwa urahisi ” amesema  Kapinga.

Hata hivyo Kapinga amesisitiza  kuwa Tume ya Ushindani wa Udhibiti wa Bidhaa pamoja kudhibiti bidhaa feki wameweka mikakati ya kuongeza ufanisi na ubunifu ili kuboresha utendaji kazi wa FCC.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa FCC,Hadija Kasongwa,amesema  tume hiyo inaratibu zaidi ili kwenda na falsafa ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuwezesha vyombo hivyo kutatua matatizo ya wananchi  katika ufanyaji wa biashara   

Kasongwa amesema katika miaka minne kulikuwa na falsafa ya ukuzaji uwekezaji nchini ambapo taasisi hiyo inapitia na kuchambua miamala ya miunganiko ya kampuni kwa lengo la kukuza mitaji pamoja na kuokoa ajira  kwa baadhi ya kampuni na viwanda. 

Sanjari na hayo amesema kuanzia Desemba 1,2025 kutakuwa na  zoezi la kurekodi  usafirishaji wa bidhaa zote zinazoingia nchini hivyo itasaidia kuzichunguza na kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki na zisizokidhi viwango.