Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
BENKI ya Exim imechukua hatua ya kuunga mkono utambuzi wa mapema wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuhamasisha maisha yenye afya kwa jamii.
Exim imeshirikiana na Chama cha Kisukari Tanzania (Tanzania Diabetes Association TDA), kuunga mkono shughuli za kitaifa za Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani 2025, ikiwa ni ishara ya dhamira yake ya kuchangia kikamilifu katika jitihada za afya ya jamii, nje ya huduma zake za kifedha.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu, amesema
“Wafanyakazi na wateja wetu ndio kiini cha kila tunachofanya, afya ni msingi muhimu wa ustawi na tija kwa kutoa vipimo hivi, tunalenga kuwapa wafanyakazi na wateja wetu elimu inayohitajika kujikinga na athari zinazohusiana na kisukari.”
Alisisitiza pia kuwa vipimo hivyo vimeendeshwa na wataalamu na kwa kuzingatia usiri wa taarifa za kiafya kwa wote walioshiriki.
Kwa kuonesha msisitizo wa kuboresha ustawi wa jamii na wafanyakazi katika maeneo ya kazi kwa ujumla, Benki ya Exim imefanya zoezi la upimaji wa kisukari bure kwa wafanyakazi na wateja wake, huku zoezi hilo likiwa limeandaliwa kwa ushirikiano na Chama cha Kisukari Tanzania, ambacho kina utaalamu katika elimu, kinga na usimamizi wa ugonjwa wa kisukari.

Imeelezwa kuwa, mpango huo unaendana na kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani mwaka huu, “Kisukari na Ustawi Mahali pa Kazi,” inayosisitiza umuhimu wa kutambua mapema, huduma za kinga na mitindo bora ya maisha, ili kupunguza hatari za kuendelea kupata ugonjwa huo.

Kwa kuleta huduma hii moja kwa moja kwa wafanyakazi na wateja, Benki ya Exim imewapa wateja na wafanya kazi wao fursa ya kujua hali zao za kiafya, kutambua viashiria mapema na kuchukua hatua za kujilinda au kujua namna ya kusismamia ugonjwa huo ikiwa umegundundulika kuwa umeathirika.
Aidha ikielezwa kuwa, uchunguzi huo ulijumuisha vipimo mbalimbali ikiwemo, Tathmini ya mtindo wa maisha (mlo, unywaji pombe, uvutaji sigara na kiwango cha mazoezi), Kipimo cha BMI, uzito na urefu, Ufuatiliaji wa shinikizo la damu na Kipimo cha sukari mwilini kwa kutumia glucometer.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi