Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Kilolo, Rita Kabati (CCM) amesema katika Bunge hili jipya anaamini yatakuwepo mabadiliko makubwa yatakayolenga kuleta maendeleo kwa wananchi, hususan katika sekta ya miundombinu ya barabara ambazo zimekuwa kero kubwa kwa wananchi hapa nchini wakiwemo wa Jimbo lake.
Akizungumza Leo Novemba 11,2025 na waandishi wa habari Bungeni jijini Dodoma, Kabati alisema amejipanga kuhakikisha changamoto zote alizoambiwa na wananchi wa vijiji mbalimbali jimboni kwake zinapatiwa ufumbuzi kupitia jitihada za kibunge na ushirikiano na Serikali.
“Nyie ni mashahidi, nilipokiwa Mbunge wa viti Maalum nimekuwa mbunge wa kwanza kuuliza maswali mengi Bungeni, na yote yalikuwa na maslahi kwa wananchi. Hilo limewajengea wananchi imani kubwa kwangu kwa sababu waliona ninachokizungumza kinawahusu moja kwa moja,” alisema Kabati.
Mbunge huyo aliongeza kuwa wananchi wa Kilolo sasa wana imani zaidi kwake, wakiamini kuwa yale aliyokuwa akiyazungumzia wakati wa kampeni sasa anakwenda kuyatekeleza kwa vitendo.
Akizungumzia changamoto kuu inayolikabili jimbo hilo, Kabati alisema tatizo kubwa ni barabara ambazo hazipitiki kabisa hasa wakati wa mvua, jambo linalokwamisha shughuli za kiuchumi na kijamii.
“Jimbo letu la Kilolo changamoto kubwa ni barabara. Wakati wa mvua hazipitiki kabisa. Niliahidi wakati wa kampeni kwamba nitahakikisha maeneo korofi yanayofanya barabara zifungwe muda wote yanaanza kufanyiwa matengenezo. Tayari upembuzi yakinifu umeshafanyika, na ninakuja kuanza kazi mara moja,” alisema.
Mbunge huyo alisisitiza kuwa dhamira yake ni kuhakikisha ahadi alizotoa zinatimia ili kuendeleza imani ya wananchi kwake na kuonyesha mfano kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa uongozi.
“Nakuja kazini kuhakikisha kwa imani niliyopewa na wananchi nawawatumikia ipasavyo. Tunataka tuendelee kuwaaminisha wananchi kwamba wanawake tunaweza, na kwa kufanya kazi vizuri, majimbo yanayoongozwa na wanawake yaongezeke zaidi,
” aliongeza kama ambayo Rais wetu Dkt.Samia anavyoonyesha katika utendaji wake kwamba wanawake wanaweza basi wabunge wanawake wote hasa wa majimbo tufanye kazi hiyo kwa uaminifu na kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi