Na Zuhura Zukheir, TimesMajira Online, Iringa
MGOMBEA Ubunge katika Jimbo la Mafinga, Cosato Chumi ameendelea kuiomba Serikali kuruhusu wananchi kufanya biashara saa 24 kutokana na mji huo kupokea wageni wengi muda wote wa mchana na usiku.
Akizungumza wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika jimbo la Mafinga kuomba kura kwa wananchi uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa, Chumi amesema kuwa, ili kukuza uchumi kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini, wanatakiwa kufanya shughuli za kimaendeleo kwa masaa yote bila kuwa na hofu ya usalama wao.
Chumi ambaye anayetetea nafasi yake, amesema kuwa ikiwa Serikali ilikubali kuruhusu malori kusafiri saa 24, anaamini chini ya uongozi wa Dkt. John Magufuli itaridhia wananchi wa Mafinga wafanye biashara hali itakayosababisha kukuza pato la mtu mmoja mmoja, pato la Halmashauri na pato la Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa, Mafinga ni Mji wa kibiashara, kitendo cha wafanya biashara kufanya kazi zao hadi saa nne na Polisi kuwazuia si sawa, hivyo kama atachaguliwa kuwa mbunge ataongoza hoja ya kubadilisha sheria ili watu waruhusiwe kufanya biashara usiku na mchana.
“Ndugu zangu Wananchi wa Mafinga wakiruhusiwa kufanya kazi, au kufanya biashara saa 24 itaongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, pato la Halmashauri na Taifa kwa ujumla hivyo naona nina wajibu wa kwenda kulipigia kelele, ” amesema Chumi.
Akiendelea kutoa hoja zake kwa wananchi, Chumi amesema kuwa, katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake amefanikiwa kuboresha sekta ya afya kwa kuwatafutia vifaa tiba pamoja na magari matatu ya wagonjwa gari moja ikiwa katoa yeye mwenye kwa kushirikiana na ofisi ya Chama cha Mapinduzi huku wananchi kuendelea kuwa na Imani na CCM
Chumi amesema kuwa, wakati anaingia madarakani mwaka 2015 alikuta hospitali ya Mafinga inayohudumia wakazi wa Wilaya yote ya Mufindi na Mbalali ilikuwa katika hali mbaya baada ya kukuta wakina mama wajawazito walikuwa wanalala chini kutokana na kukosekana kwa vitanda
Amesema, hali hiyo ilitokana na bajeti finyu iliyokuwa iletwa kwa ajili ya hospitali ukilinisha idadi ya watu wanaohudumiwa hali iyomsukuma kupeleka hoja bungeni na serikali iliunga mkono hoja hiyo kwa kutenga bajeti ya kujenga kituo cha afya Ihongole ili kupunguza msongamano.
Katika kipindi chake cha miaka mitano pia amefanya juhudi kama mbunge kwa kushirikiana na wadau amefanikiwa kujenga jengo la upasuaji lenye vyumba vitatu na sehemu ya kupumzikia katika hospitali hiyo ya Mafinga huku katika kata mbalimbali tayari kumeanza ujenzi wa vituo vya afya. kwa juhudi zake katika kuishawishi serikali hivyo zawadi pekee kwa chama cha mapinduzi nikumpa kura za kutosa Rais Magufuli, kura nyingi kwa mbunge wa CCM na madiwani wake.
Kwa upande wa sekta ya elimu amesema kuna wajibu wa kumshukuru rais Magufuli kwa kumpa kura za heshima kutokana na kuleta fedha kiasi cha billion 3 na million 500 kwa mafinga kwa ajili ya kutoa elimu bure huku fedha zingine kiasi cha shilingi Billion 1 na milioni 900 kwaajili ya kuimarisha miundo mbinu ya shule kama Makalala ambako kwa sasa wanaishi na kusoma katika mazingira Rafiki huku changalawe akiwa amesaidia kiasi cha shilingi 400 kwaajili ya ujenzi wa jiko na bwalo la chakula.
Akigusia sekta ya maji, Chumi amesema kuwa, anawaomba wananchi wampe kura nyingi za kutosha ili akipita na kuwa mbunge atahakikisha ndani ya miaka miwili vijiji vyote vilivyobaki vitakuwa vimepata maji
Amesema, miaka mitano iliyopita amefanikiwa kusaidia ujenzi wa mabweni katika shule mchanganyiko ya mkalala sambamba na kuunganisha mfumo wa maji ya moto ili Watoto wanaosoma pale waweze kupata huduma nzuri
Kuhusu umeme Chumi amesema, alikuwa akimsumbua Waziri wa Nishati kwa ajili ya kusogezewa umeme katika vijiji na tayari vijiji vingi vimewaka umeme na vilivyobakia ataenda kuvipigia kelele ili vyote vipate umeme.
More Stories
TCC yaibuka kidedea tuzo za PMAYA
Mwanafunzi apoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba
Mwanafunzi adaiwa kuuwawa na rafiki wa baba yake