March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MNEC Dkt.Angeline ajitokeza kupiga kura

Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MNEC),Dkt.Angeline Mabula, ameungana na wananchi wa Kata ya Kirumba na taifa kwa ujumla,kujitokeza kupiga kura la kuchagua viongozi katika nafasi ya urais,ubunge na udiwani.

Dkt.Angeline,amefika mapema leo Oktoba 29,2025,katika kituo cha kupigia kura cha Kirumba Kati C1,Kata ya Kirumba jimboni Ilemela mkoani Mwanza,akiwa miongoni mwa wapiga kura wa kwanza kushiriki katika zoezi la kupiga kura kituoni hapo.

Baada ya kutekeleza haki yake ya kidemokrasia na kikatiba,Dkt.Angeline ametoa wito kwa wananchi  kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kupiga kura, akisisitiza kuwa ni fursa muhimu ya kuchagua viongozi wanaostahili kuwatumikia huku hali ya usalama ikiwa ni shwari.