Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imeendelea kusambatratisha mitandao ya Dawa za kulevya nchini, kutokana na Operesheni zake kabambe kuleta matokeo chanya.
Lengo la kufanya Operesheni hizo ni kulinda afya za Watanzania, vizazi vijavyo pamoja na nguvu kazi ya taifa.
Katika kipindi cha mwezi wa mwezi Septemba na Oktoba 20256, Mamlaka hiyo imekamata jumla ya kilo 10, 763.94 za dawa za kulevya aina mbalimbali, ikiwemo kilo 6,007 na lita 153 za kemikali bashirifu.
Operesheni hiyo ilifanyika katika maeneo mbalimbali nchini, huku watuhumiwa 89 wakitiwa nguvuni kuhusiana na uhalifu huo.

Hayo ameyasema Oktoba 21,2025 na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali Lyimo, amesema mafanikio hayo sehemu ya mapambano endelevu dhidi ya dawa za kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
“Dawa za kulevya si tu zinaharibu afya ya mtumiaji bali zinatishia usalama wa taifa, uchuni pamoja na nguvu kazi ya taifa ikiwemo vijana, hivyo hatutasita kumchukulia hatu yeyote atakayehusika na biashara hiyo haramu,” amesema Kamishna Jenerali Lyimo.
Aidha, amesema walifanya Operesheni eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, na kufanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya mirungi iliyokaushwa na kufungwa kama
viungo (spice), yenye uzito wa kilo 40.32.
“Dawa hizi zilikuwa kwenye paketi 80 zenye maandishi ‘dry basil leaves’ na zilikuwa tayari kusafirishwa kwenda Canada na Italy.

“Watuhumiwa wa wanaohusiana na tukio hilo ni Yusuphu S Kibaha mwenye umri wa miaka 35 na Mohamed H. Ramadhani mwenye umri wa miaka 41 tayari tumeshawakamata,” amesema Kamishana Lyimo.
Hata hivyo amesema, taarifa za uchunguzi zimebainika kuwa, dawa hizo za kulevya ziliingizwa nchini kwa njia ya kificho kutokea nchi jirani na zilitumwa kupitia Makampuni ya usafirishaji.
Aidha, amesema Mamlaka imebaini kuwepo mtandao wa usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi, ambao hutumia bodaboda wakishirikiana na mawakala wa kampuni sa usafirishaji nchini, ili kurahisha biashara yao.
Katika tukio jingine ambalo liliwashangaza wengi, DCEA ilifanya Operesheni katika eneo la Mlalakua Kinondoni jijini Dar es Salaam, iligundua kuna kundi la vijana ambao wanatengeneza biskuti za bangi kwa ajili ya house party ya wanafunzi wa vyuo Vikuu.
Mara baada ya kubaini hilo, Mamlaka iliwakamata watuhumiwa Bright A. Malisa, Humphrey G. Safari, Novatus A. Kileo na Chriss P. Mandoza wote wakiwa na umri wa miaka 26.
Kamisha Jenerali Lyimo amesema vijana hao walikutwa na biskuti 140 za bangi, puli nane na paketi tisa za bangi zenye jumla ya kila 2,858.

“Natoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kotojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kwani hatari kwa kizazi kijacho lakini pia, natoa wito kwa wazazi kufuatili mienendo ya watoto wao pindi wanapokuwa vyuoni.
“Kuanzia sasa tutafuatilia house paty zote zinazofanywa na wanafunzi wa vyuoni na zikibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” amesema.
DCEA pia, ilifanya operesheni katika mkoa wa Mikoa ya Morogoro, Simiyu, Arusha, Kilomanjaro, Mwanza, Tanga, Pwani, Shinyanga, Ruvuma, Tabora na Mtwara na kufanikiwa kukamata bangi kilo 9, 164.92.
Kamishna Lyimo alisema, pia walikamata mirungi kilo 1,555.46, skanka gramu 367 na heroin gramu 7.498 pamoja na kuteketeza ekari 11.5 za mashamba ya bangi.
Mamlaka imeta wito kwa wale wote wanahusika na biashara pamoja na matumizi ya dawa za kulevya kuacha mara moja, lengo ni kuhakikisha Tanzania inabaki salama na huru kwani bila ya dawa za kulevya inawezekana.


More Stories
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani