Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo, ameendelea na ziara yake ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Katika ziara hiyo, Fyandomo ameshirikiana na wagombea ubunge wa majimbo yote mkoani humo, akiwahimiza wananchi kutokosa nafasi yao muhimu ya kuchagua viongozi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amekuwa akizungumza nao moja kwa moja katika masoko, vijiweni, maduka ya nyama, saluni za kike, gereji, vilabu vya pombe za kienyeji pamoja na kwa wajasiriamali wadogo. Katika mikutano hiyo, ameeleza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020–2025 na malengo mapya kuelekea mwaka 2025–2030.
“Ndugu zangu, nimekuja kuwaomba kura za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa CCM siku ya Oktoba 29, 2025. Tafadhali msikubali kurubuniwa na maneno ya chuki,” amesema Fyandomo.
Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kudumisha amani na mshikamano, na kujitokeza kupiga kura kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni, ili kuchagua viongozi watakaoipeleka Tanzania mbele zaidi.
“Tunaona maendeleo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika sekta za afya, maji, barabara, elimu na nishati vijijini na mijini chini ya uongozi wa mwanamama shupavu, Dkt. Samia “amesisitiza.
Aidha Fyandomo amewataka wanawake na vijana, madereva wa bodaboda, bajaji, mama lishe na baba lishe — Jumatano hiyo tujitenge muda wa kwenda kutiki kura kwa Rais, Wabunge na Madiwani wetu,.


More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi