Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT WAZALENDO, Othman Masoud Othman, amesema mara atakapochukua madaraka ya Urais wa Zanzibar atawajengea uwezo wasanii wa ndani ili waweze kufikia viwango vya kimataifa na kuitangaza Zanzibar duniani kupitia vipaji vyao.
Amesema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wambaa, Jimbo la Chambani, Mkoa wa Kusini Pemba, ambapo alisisitiza kwamba Zanzibar imebarikiwa kuwa na vipaji vingi vya sanaa ikiwemo muziki, filamu, uchongaji na sarakasi.

“Zanzibar ina hazina kubwa ya wasanii. Kinachokosekana ni mazingira bora ya kuwawezesha. Serikali nitakayoiongoza itahakikisha sanaa inakuwa ajira rasmi na chanzo cha kipato,” amesema Othman.

Aidha, Othman amebainisha kuwa serikali ya ACT Wazalendo itaunda mfuko maalum wa maendeleo ya sanaa, kukuza ubunifu na kutoa mafunzo ya kisasa kwa vijana wenye vipaji, akisisitiza kwamba lengo ni kuona Zanzibar ikitambulika duniani kupitia sanaa na utamaduni wake.

More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro