Mbunge ataka mpango wa matumizi bora ya ardhi
Na Joyce Kasiki,Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalum Hawa Mwaifunga (CHADEMA) amesema mwarobaini pekee wa kumaliza migogoro ya ardhi nchini ni kupanga matumizi bora ya ardhi.
Akizungumza feb 8,2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala kuhusu utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii kwa mwaka 2023,Mwaifunga amesema hatua hiyo itawafanya wananchi kugusa maeneo ambayo siyo ya kwao.
“Nimwambie tu Mheshimiwa Waziri (Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Slaa) hii migogoro anayokwenda kutatua leo,kesho itazinguka migogoro mingine,maana Taifa hatujaamua kupanga matumizi bora ya ardhi,kila iitwapo kesho tutakwenda kuwa na migogoro,
“Mheshimiwa mwenyekiti hii nchi inahitaji kupangiwa matumizi ya ardhi ,tukiwa na matumizi bora ya ardhi watu hawagusi eneo ambalo siyo la kwao kama hautapanga matumizi bora ya ardhi,hatutafanya kitu na hii migogoro haitakwisha .”amesema Mwaifunga na kuongeza kuwa
“Safari hii kama hakutakuwa na bajeti ya kutosha ya Tume ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ,na mimi nitakuwa mmoja kati ya wabunge ambao hatutapitisha bajeti ya Wizara ya ardhi,kwa sababu haiwezekani tuwe tunashauri Serikali halafu haitekelezi wakati sisi ndio wenye changamoto hizo tunatoka nazo kwa wananchi wetu.”Â
Aidha amesema mkoa wa Tabora ndiyo mkoa wenye eneo kubwa Tanzania huku akisema mkoa wa Tabora uwe ni miongoni mwa mikoa itakayopunguzwa ili wananchi wa mkoa huo waweze kupata maendeleo.
“Nimuombe sana Mheshimiwa Waziri katika kliniki unazoendelea nazo,naomba mkoa wa Tabora upewe kipaumbele ili kupunguza matatizo na changamoto za ardhi kwa wananchi.”amesema
Kwa mujibu wa Mwaifunga Tabora ardhi ni kubwa na kwamba matajiri wachache wanakwenda kununua ardhi kwa ajili ya kuihodhi na baadaye aanze kuuzia wengine.
“Jambo hili ni baya,kama tungekuwa tumeshapanga matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo yetu,tungejua mama hapa pangejenwa shule,hospitali ,kituo cha afya,leo mheshimiwa Rais Samia Duluhu Hadsan anashusha fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo,lakini unakuta hakuna maeneo ya kujenga kwa sababu kuna watu wanahodhi hayo maeneo na anayeanza kwa bei anayotaka yeye.”
Amesema hatua hiyo inasababisha wananchi kutafuta maeneo ambayo yapo wazi na kujimilikisha na hivyo kutengeneza migogoro ya ardhi.
Aidha Mwaifunga ameonesha kukerwa na kitendo cha maeneo ya kihisitoria mkoani humo kutelekezwa.
“Tuna eneo moja la Taasisi pale Tabora lipo katikati ya mji,pale Luna sanamu ya mwalimu Nyerere ,katuka eneo hilo mwaka 1958 mwalimu Nyerere alicia machozi akiomba uhuru wa nchi hii,sasa ukiona eneo lile ni changamoto kubwa halina umeme,majengo yamechakaa,hiyo sanamu yenyewe ya mwalimu Nyerere imechakaa unajiuliza kama nyinyi watu wa Wizara ya Maliasi,mna makumbusho,Malikale mnashindwa hata kututengenezea eneo ambalo mwali Nyerere alilia machozi wakati akiomba uhuru wa Taifa hili,
“Mnashindwa kulifanya eneo hili kuwa la makumbusho,mnafanya mini kwenye wizara,nimeongea kwa uchungu maana mnatuchosha mnaufanya moka wetu unazidi kuwa mkongwe ,moka wa Tabora umefunguka,tuwekeeni makumbusho ili vizazi na vizazi vijue moka wa Tabora umechangia katika uhuru wa Taifa hili.”
Ameipongeza Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA) ambao hivi sasa wameanza kutengeneza maeneo ya vivutio mkoani Tabora.
Kuhusu mabaraxa ya Ardhi amesema bado ni kero kwa wananchi kwani yanayosababisha migogoro kila siku.
More Stories
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao