Na Heri Shaaban, Timesmajira Online
MAKADA 38 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala wamejitosa katika kinyanganyiro cha kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho nafasi ya Ubunge katika majimbo manne ya wilaya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa CCM wilaya ya Ilala Chief Silivester Yared,amesema zoezi la kutoa fomu limeanza Juni 28 mpaka Julai 2 mwaka huu ambapo mwitikio umekuwa mkubwa kwa makada wa chama hicho.

Ambapo amesema tangu kuanza kwa zoezi hilo wameisha jitokeza makada 38 katika majimbo manne yanayopatikana wilayani Ilala,kati yao Jimbo la Kivule 22,Ukonga watatu,Ilala watano na Segerea watano.
Yared amesema kati ya wagombea 38 waliojitokeza wanawake saba na wanaume 31 wote wamechukua fomu katika kinyanganyiro hicho cha kura za maoni kwa ajili ya mchakato ndani wa CCM.
Sanjari na hayo amesema,kwa upande wa nafasi ya Udiwani waliochukua fomu ni 134 kati yao wanawake 29 na wanaume 105.
Kwa upande wao baadhi ya watia nia waliochukua fomu za kuwania nafasi za Ubunge na Udiwani,wameeleza sababu za kutaka kugombea nafasi hizo.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Kivule,Frolian Karugaba,ambaye ni miongoni mwa kada wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu katika mchakato wa kura za maoni kwa ajili ya kupata mtu atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu kwa nafasi ya Ubunge jimboni humo,amesema sababu ya kujitosa ni kutaka kutatua changamoto mbalimbali za wanakivule.

Huku Mjumbe wa Baraza la Wazazi Taifa Saady Kimji,amechukua fomu kwa ajili ya nafasi ya Udiwani Kata ya Ilala akitetea kiti hicho kwa awamu ya tatu.Huku Nyansika Getama, amechukua fomu ya Udiwani Kata Kivule

More Stories
Serikali inatambua uwepo wa Watumishi wachapa kazi na uweledi
DED Mweli:Tumeweka kipaumbele kusikiliza kero za wananchi
CHAKUWAHATA wawagusa wanafunzi wa kike