Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama amewataka watumishi wa Umma kufanya Kazi kwa kujituma kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo Mhagama amesema,endapo watumishi wakifanya Kazi vizuri inamUhamasisha Rais Samia Suluhu Hassan kujibu hoja zinazowakabili watumishi wa Umma kwa vitendo.
“Zawadi pekee kwa watumishi wa Umma ya kumpa Rais (Samia Suluhu Hassan) ni kiwajibika kwa vitendo…,unajua kadri tunavyokuwa tunawajibika tunampa hamasa Rais kujibi hoja za watumishi wa Umma kwa vitendo.”amesema Waziri Mhagama na kuongeza kuwa
“Mimi natamani mtumishi wa Umma aipende Kazi hadi siku akikosa kwenda kazini akipimwa akutwe’ temperature'( joto) imepanda.”
More Stories
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini