January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bondia wa Uingereza atua nchini

Na Yusuph Digossi, TimesMajira Online

BONDIA kutoka nchini Uingereza John Brennan ametua hapa nchini leo asubuhi kwa ajili ya pambano lake litakalofanyika kesho Oktoba 16 dhidi ya Mtanzania Issa Mbwana .

Issa atamkaribisha Muingereza huyo katika pambano lisilo la ubingwa la raundi nane uzito wa kilogramu 69.85 Super Welterweight katika mapambano ya wazi yatafanyika katika Uwanja wa Mabembeauliopo Keko Magusumbasi na hayatakuwa na kiingilo.

Tayari Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) lilishapokeo mikanda yote ya ubingwa kuelekea kwenye mapambano hayo ya ‘Open Air International Boxing’.

Sababu za bondia huyo kuwasili hapa nchini siku moja kabla ya pambano lake imeelezwa kuwa ni kuogopa hujuma na mbinu za michezo kwani anachokitaka na kuondoka na ubingwa huo.

Katibu Mkuu wa PST, Anthony Rutta amesema, mara baada ya kutua hapa nchini, moja kwa moja bondia huyo atakwenda kupima uzito tayari kwa pambano hilo litakalofanyika kesho.

Amesema, maandalizi yote kuelekea kwenye pambano hayo yameshakamilika na leo mabondia watapima uzito na afya tayari kwa ajili ya kupanda ulingoni.

Mbali na bondia huyo, lakini pia mabondia mwingine kutoka nje ya nchi akiwemo Prince Patel kutoka Uingereza amewasili nchini juzi tayali kukabiliana na Mtanzania Innocent Everist katika pambano la kugombea mkanda ubingwa wa WBO ‘WBO Global & Africa’ katika pambano la raundi 12 uzito wa kilogramu 52.16 Super Flyweight.

Katika mapambano hayo pia bondia wa kike, Halima Vinjabei atapanda ulingoni kupambana na mpinzani wake kutoka nchini India katika pambano la raundi 10 uzito wa kilogramu 48.98.

Mabondia kutoka Tanzania Julias Kisarawe na Salum Msabaha watawania ubingwa wa UBO All Africa and PST katika pambano la raundi 10 uzito wa kilogramu 52.16 Super Flyweight huku watanzania Singa Chala na Yusuph Shamsani wakipigana raundi nne.