May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwendesha baskeli akikatisha ukuta wa baskeli iliowekwa kama kizuizi, katika zuio la kutoka nje (lockdown) la siku 21 ambalo linatekelezwa nchini humo ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa (COVID-19), Mumbai, India hivi karibuni.

New Delhi

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ameongeza marufuku ya kutoka nje (lockdown) ili kuendelea kupunguza kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona, hata hivyo ongezeko hilo la muda halikusema litaishia lini.

Kwa mujibu wa Reuters, mapema Modi alifanya mkutano na mawaziri wa majimbo nchini humo kwa njia video, kuzungumzia hatma ya marufuku hiyo huku akiungwa mkono na viongozi hao. “Amechukua hatua sahihi kuongeza muda” alisema Waziri Arvind Kejriwal, ambaye ni waziri wa New Delhi

“Kama marufuku ingeishia leo, mafanikio yote yangepotea. Kwa maana hiyo ni vyema muda ukuongezwa ” Kejriwal aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

India imeingia katika marufuku hiyo ya siku 21 ambayo inatakiwa kuisha jumanne ijayo, hata hivyo viongozi wa majimbo mbalimbali wamemtaka Modi kuongeza muda, hata baada ya mamilioni ya raia wa nchi hiyo  kulalamikia hatua katazo la kutoka nje kutokana na umaskini mkubwa, huku watu wa kipato cha chini wakilazimika kukimbilia vijijini ili kujikwamua na ugumu wa maisha.