New Delhi
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ameongeza marufuku ya kutoka nje (lockdown) ili kuendelea kupunguza kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona, hata hivyo ongezeko hilo la muda halikusema litaishia lini.
Kwa mujibu wa Reuters, mapema Modi alifanya mkutano na mawaziri wa majimbo nchini humo kwa njia video, kuzungumzia hatma ya marufuku hiyo huku akiungwa mkono na viongozi hao. “Amechukua hatua sahihi kuongeza muda” alisema Waziri Arvind Kejriwal, ambaye ni waziri wa New Delhi
“Kama marufuku ingeishia leo, mafanikio yote yangepotea. Kwa maana hiyo ni vyema muda ukuongezwa ” Kejriwal aliandika katika mtandao wake wa Twitter.
India imeingia katika marufuku hiyo ya siku 21 ambayo inatakiwa kuisha jumanne ijayo, hata hivyo viongozi wa majimbo mbalimbali wamemtaka Modi kuongeza muda, hata baada ya mamilioni ya raia wa nchi hiyo kulalamikia hatua katazo la kutoka nje kutokana na umaskini mkubwa, huku watu wa kipato cha chini wakilazimika kukimbilia vijijini ili kujikwamua na ugumu wa maisha.
More Stories
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang
Daktari Dar ajishindia Mil. 100/- za Fainali NMB Bonge la Mpango