Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Diana Bundala maarufu Mfalme Zumaridi(42),Mkazi wa Buguku kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana anashiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kuendesha shughuli za kidini bila usajili pamoja na kufanya mahubiri kwa sauti ya juu.
Akizungumza jijini hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa,amesema,Mei 15,2025 majira ya saa nne asubuhi huko mtaa wa Buguku, kata ya Buhongwa, wilaya ya Nyamagana,walimkata Zumaridi,ambaye anatuhumiwa kuyageuza makazi yake kuwa kanisa na kuendesha shughuli za kidini bila usajili.
Ambapo anatuhumiwa pia kufanya mahubiri kwa waumini wake kwa sauti ya juu katika eneo hilo ambalo ni makazi ya watu na kusababisha usumbufu kwa majirani wanaoishi karibu na makazi yake.
Mutafungwa amesema,pia Zumaridi anahojiwa kuhusiana na taarifa inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii akionekana kwenye picha mjongeo akiwa na kundi la watoto wenye umri mdogo wa jinsia ya kike na kiume akiwaeleza kuwa yeye ndiye Mungu wao ambaye ana uwezo wa kuwatenganisha na kifo.
Amesema,uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea,ambapo jeshi hilo litashirikiana na taasisi nyingine za serikali,hivyo linawaomba wananchi wenye taarifa mbalimbali zinazoweza kusaidia uchunguzi wa tuhuma hizo wazifikishe polisi.Hata hivyo uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.
More Stories
Doreen: ‘Msiwafiche watoto wenye utindio wa Ubongo
Serikali yawezesha miradi 80 kwa utaratibu wa PPP
Mpogolo akabidhi Cheti kwa wahitimu