Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki anayefanya vizuri katika kiwanda cha Bongo fleva, Zuhura Othman Soud maarufu kama ‘Zuchu, leo amewasaidia Kinamama waliopo mji mpya wa Kwahani kibanda hatari uliopo kisiwani Unguja.
Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Zuchu amesema, amefanya hivyo baada ya kutambua umaskini unaowagusa wanawake kutokana na majukumu mazito hasa ulezi wa familia.
”Mimi Kama binti nilielelewa na ‘Single Mother’ Pekee, natambua dhahiri kua Wimbi la unyonge na Umaskini huwagusa zaidi Wanawawake kutokana na majukumu Mazito ya ulezi Wa familia.
“Na Kwa kutambua hili, leo Julai Mosi nimekuwa nanyi ndugu zangu kwa ajili ya Kugawana Kidogo Changu nilichojaaliwa Kwa WakinaMama Wasiopungua 100.
“Ukimsaidia Mwanamke umeisaidia Jamii.Kutoa ni moyo, Mchango wangu huu hauna lengo la kubagua jinsia hapana, Ila tu kwa sasa ningependa sana nianze na wakina Mama,” amesema Zuchu.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio