Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa kike anayekuja kwa kasi hapa nchini katika tasnia ya muziki wa Bongo fleva kutoka lebo ya WCB, Zuhura Kopa maarufu ‘Zuchu’, amesema amefurahi sana kuhudhulia kwenye tukio la kuapishwa kwa rais wa Zanzibar awamu ya nane Hussein Ally Mwinyi lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa Amani Zanzibar.
Katika sherehe hiyo, Zuchu alipata nafasi ya kuwatumbuiza wananchi wa Zanzibar, pamoja na wageni mbalimbali waalikwa waliohudhulia baada ya Mwinyi kushinda kwenye Uchaguzi mkuu uliofanyika viziwani Zanzibar na kufanikiwa kuwa mtawala wa visiwa hivyo.
“Asante Sana kwa Serikali yangu kwa kuendelea kuona Mchango Wangu. Nimefurahi Sana kuwepo Kwenye Tukio Hili La Kihistoria,” ameandika Zuchu kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA