Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Wanawake wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kata ya Zingiziwa wameadhimisha siku 16 za kupinga ukatili Duniani kwa kufanya maandamano na wanafunzi wa Shule mbalimbali Tarafa ya UKONGA .
Madhimisho hayo ya siku ya kupinga ukatili wa kijinsia yalifanyika
Zingiziwa Sokoni Wilayani Ilala .
Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawanchi Kiuchumi Kata Zingiziwa Nipael Joshua, alisema Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,jinsia wanawake na Makundi maalum imeandaa miongozo wa uwanzishwaji na uendeshaji la jukwaa uwezeshaji Wananchi Kiuchumi .
Nipael alisema katika madhimisho hayo ya kupinga Ukatili Jukwaa Zingiziwa tunashirikiana na Chama na Serikali katika mitaa minane ya Zingiziwa kukemea vitendo vya kupinga Ukatili na kuyatolea taarifa ngazi ya mitaa mpaka Dawati la jinsia
Aidha alisema wanapata ushirikiano mkubwa kutoka kituo Cha Polisi CHANIKA kutokana na matukio ya vitendo vya ukatili
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM kata ya Zingiziwa Omary Mlewa ,alipongeza Wanawake wa Zingiwa wa Jukwaa la Wanawake kuadhimisha Siku hiyo ya madhimisho ya kupinga vitendo vya ukatili
Katibu Mlewa alisema wazazi Wana jukumu kubwa Sana kukemea vitendo vya ukatili katika kuisaidia Serikali kila wakati inatakiwa kupinga na kukemea .
Mlewa aliagiza jeshi la Polisi Chanika wakikamata mtu au watu wenye vitendo vya ukatili wachukuliwe hatua za kisheria wasiwafumbie macho.
Kwa upande wa Jeshi la Polisi INSP .Bonevetura Bushumba alisema vitendo vya Ukatili vinalenga kwa wanawake sababu Wanawake ni viumbe Dhaifu sera ya kuzuia Ukatili Chanika na Zingiziwa matendo ya Ukatili yakitokea unatakiwa KUTOA taarifa .
Kamanda Bonevetura alisema mzazi ana jukumu la kukemea vitendo vya kupinga Ukatili Ili Mtoto asifanyiwe Ukatili Zingiziwa na Gogo wametakiwa kutumia majukwaa KUTOA taarifa na kukemea pia aliwataka washirikiane na SERIKALI .
More Stories
15 mbaroni tuhuma wizi wa shehena ya unga wa sembe
Wacheza rafu Uchaguzi Mkuu ujao waonywa
Hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wanaohatarisha usalama Mbeya