December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ziara ya Rais Samia kuacha alama isiyofutika mkoani Morogoro

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Moro

RAIS Samia Suluhu Hassan leo anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku sita katika Mkoa wa Morogoro, huku akiacha alama nne zitakazobaki kama kumbukumbu kwa wakazi wa mkoa huo.

Katika ziara hiyo iliyoanza Agost 2, mwaka huu Pamoja na mambo mengine mkuu huyo wa nchi alizindua Kampeni ya ‘Tutunzabe Mvomemero 2023-2028,’Daraja la Berega lililopo na kuwapatanisha wakulima na wafugaji kwa kuwataka wapeane mikono kama ishara ya kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji.

Rais Samia amezindua kampeni hiyo wilayani Mvomero mkoani Morogoro Agosti 3, 2024.

Wakati akizindua kampeni hiyo, Rais Samia alisema mradi huo wa kuhamasisha ufugaji wa kisasa una umuhumu mkubwa kwa wafugaji na jamii inayowazunguka. “Kampeni hii ni muhimu kwetu kwa sababu inakwenda kuleta amani, kuleta ongezeko la malisho, tija na wafugaji kuweza kukopesheka”, alisema Rais Samia.

Aliongeza kwa kusema kuwa kampeni hiyo itasaidia pia kutunza mazingira na kuepusha athari zake, huku akiwataka wakulima na wafugaji kuheshimiana kwa sababu wote wanategemeana.

Aidha, Rais Samia alitoa pongezi kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Serikali ya Mkoa wa Morogoro kwa ubunifu wao, huku akiwaahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuiunga mkono kampeni hiyo ya mfano hapa nchini.

Alifafanua kuwa sekta za mifugo na kilimo zimeajiri watu wengi nchini na kwa sababu hiyo ataendelea kuweka msukumo ili kampeni hiyo iweze kuleta mabadiliko na mapinduzi makubwa kwa wafugaji na wakulima ili kuwainua na kuwanufaisha wananchi walio wengi.

Halikadhalika aliwaeleza wafugaji na wakulima kuwa mabadiliko hayaepukiki, hivyo ni muhimu wakaunga mkono kampeni hiyo ili waweze kuepukana na migogoro ya kila uchao.

Akizungumzia mradi wa Tutunzane Mvomero, Rais Samia alisema kuna haja wafugaji kufanya ufugaji wa kisasa ikiwemo kuwa na maeneo yao ya kulima malisho ili kuondokana na migogoro kati yao na wakulima na watumiaji wengine wa ardhi kila uchao.

“Kampeni hii ni muhimu kwetu kwa sababu inakwenda kuleta amani, kuleta ongezeko la malisho, tija na wafugaji kuweza kukopesheka”, alisema Rais Samia.

Wakati akizindua kampeni hiyo Rais Samia alisema mradi huo wa kuhamasisha ufugaji wa kisasa una umuhumu mkubwa kwa wafugaji na jamii inayowazunguka.

Aliwataka kuwasimamia wenyeviti wa vijiji waache kunyoosha mikono ,na walete suluhu za kweli nacsheria lazima zifuatwe.

Rais Samia pia alimtaka kila mwananchi kuheshimu Uhuru wa mwenzake kwa kila shughuli anayoifanya ikiwemo ya kilimo na ufugaji, kwani wote wanategemeana katika maisha ya kila siku.

Huduma ya msaada wa kisheria ikiendelea

Aliwataka wakuu wa wilaya na mikoa kuwachukulia hatua wale wote watakaoingilia uhuru wa watu kwa manufaa binafsi.

“Kila mmoja aheshimu mipaka ya mwenzie, kama unataka kulisha mifugo kalishe kwenye malisho sio kwenye mashamba, nanyie wakulima muncher kukata mifugo ya wenzenu” alisema.

Katika hatua nyingine,Rais Samia amezitaka mamlaka za mikoa na wilaya nchini kuhakikisha wanawasimamia vyema wenyeviti wa vijiji ili waache kupokea rushwa ili kuleta suluhu ya migogoro ya ardhi.

Aliwataka kuwapatanisha wakulima na wafugaji kwa kuwataka wapeane mikono kama ishara ya kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji.

“Maugomvi mwisho leo na sasa wote mnakwenda kubadilika na kuingia kwenye mradi mkabadilike, mlime mnaolima na mnaofuga mkafuge, hakuna haja ya kugombana, mtumie mradi huu ,nyie wote mnatupa uhai na mnatupa vitoweo na vyakula,” alisema.

Aliongeza kwa kusema kuwa kampeni hiyo itasaidia pia kutunza mazingira na kuepusha athari zake huku akiwataka wakulima na wafugaji kuheshimiana kwa sababu wote wanategemeana.
.
Alifafanua kuwa sekta za mifugo na kilimo zimeajiri watu wengi nchini na kwa sababu hiyo ataendelea kuweka msukumo ili kampeni hiyo iweze kuleta mabadiliko na mapinduzi makubwa kwa wafugaji na wakulima ili kuwainua na kuwanufaisha wananchi walio wengi.

Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, alimshukuru Rais Samia kwa maono yake na falsafa yake ya 4R ambayo ndio imepelekea kampeni hiyo kuanzishwa.

Vile vile Ulega alitoa shukrani za Wizara yake kwa uongozi wa mkoa na wilaya akisema “Rais, napenda pia kuwashukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero kwa kuhamasisha Kampeni hii inayoakisi maono yako ya 4R – yaani Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu) Reform (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya), katika kuleta maridhiano baina ya jamii za wafugaji na wakulima”.

Waziri Ulega aliongeza kuwa Kampeni hiyo imefanikiwa kuhamasisha wafugaji na wakulima 825 kushiriki kwa vitendo katika kampeni hii.

“Jumla ya mashamba ya wafugaji 365 yamepimwa na kutengenezewa hati, na miundomibu ya maji kwa wafugaji imejengwa ikiwemo visima sita.

Wananchi wakipata huduma ya msaada wa kisheria

Vilevile, jumla ya tani 10 za mbegu za Juncao, kilo 462 za mbegu za Rhodes na miche 10,000 ya miti ya malisho aina ya Leucaena zimegaiwa kwa wananchi ambao ni wanufaika Kampeni hii.

Katika ziara hiyo Aliahidi kufanyia kazi ombi la ujenzi wa Barabara ya Wami-Dawawa-Madizini lililotolewa na kiwanda cha Mtibwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema Serikali inatoa Sh220 bilioni ikiwa ni misamaha ya Kodi katika seta ya sukari.

Misamaha hiyo, alisema inalenga kuhakikisha sekta ya sukari nchini inaimarika, huku uzalishaji ukiongezeka. Kwa mujibu wa Bashe, Serikali kwa sasa inaandaa Sera ya Taifa ya fedha katika sekta ya kilimo ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mre

Aidha, ziara hiyo ilimfikisha Rais Samia hadi Hospitali ya Wilaya ya Gairo na kuzungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Gairo.

Sambamba na hayo, Rais Samia aliwasihi wawekezaji waendeleee kuwekeza kwenye teknolojia na mbinu za kisasa katika uzalishaji ili kupunguza gharama na kuongeza tija zaidi.

Mkuu wa nchi pia aliwata viongozi kutumia kampeni mbalimbali za suluhisho la Amani badala ya kutoa matamko. “Kilio kilichopo ni kwamba hawasimamii Serikali za vijiji, watu wakishaumizana huko ni rahisi kunyoosha mkono kupokea kuliko kuleta suluhu,” alisema.

Akizindua Daraja la Berega lililopo Wilayani Kilosa ambalo linaunganisha Wilaya hiyo na Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga, aliwataka wananchi wa Kilosa kutunza miundombinu ya Daraja hilo ili liwe chachu ya uchumi kwao na kuwaletea maendeleo.

Aidha, Rais Samia alimtaka Waziri wa Kilimo kuangalia namna ya kuwasaidia wazalishaji wa zao la mbaazi kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na bei bora zaidi.

Vile vile Rais Samia pia alizungumza na wananchi wa Dumila, ambapo alisema kuwa Serikali inaendelea kuifanya kazi migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Jambo lingine ambalo limenogesha ziara ya Rais Samia ni huduma ya msaada wa kisheria inayotolewa na wanasheria wanaoambatana na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ziara yake ya mkoani Morogoro.

Wanasheria hiyo wameendelea kuwa msaada kwa wananchi kwa kutoa elimu ya sheria na kuchukua changamoto zao kwa ajili ya kuzifanyia kazi.

Wanasheria hao wanaotoka kwenye Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid ,walianza kuambatana na Rais Samia tangu kuanza kwa ziara yake kwa lengo la kusaidia wananchi wanaotoa kero za kisheria katika ziara hiyo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria, Beatrice Mpembo, alisema wameambatana na Rais Samia ili kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria.

“Tutakuwa na Rais muda wote wa ziara hapa Morogoro na tupo na Waziri wetu, Pindi Chana na wasaidizi wa kisheria ngazi ya wilaya na mkoa, kila anapofika Rais kama kuna mtu ana changamoto ya kisheria tunaichukua na kuifanyia kazi,” alisema

“Kupitia ziara hii tumeshatoa msaada wa kisheria kwa wananchi mbalimbali na hata jamii ya wamasai tumekutana nao kwenye maeneo mbalimbali na tumewapa elimu ya sheria kuhusu migogoro yao ya mara kwa mara ya ardhi,” alisema Beatrice.

Alisema wakati wanasheria wengine wakiwa kwenye ziara hiyo, Rais Samia ametuma wanasheria wengine kupitia Kampeni ya Mama Samia Legail Aid kutoa huduma za msaada wa kisheria kwenye maonesho ya Nane nane mkoani humo.