February 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ziara ya Rais Dkt. Samia kutikisa Mkoa wa Tanga

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline

ZIARA ya Rais Samia Suluhu Hassam ambayo ataifanya mkoani Tanga ambao ni lango kuu la uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki, inatarajiwa kutikisa mkoa huo, ambapo pamojana mambo mengine atazindua na kukagua miradi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Balozi Dkt. Batilda Buriani ziara hiyo ya Rais Samia mkoani Tanga inatarajiwa kuanza Februali 28 hadi Machi 7, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Balozi Dkt. Buriani alisema kupitia ziara hiyo Rais Samia atakagua miradi, kuzindua miradi mikubwa ikiwemo mradi wa bandarai ya Tanga.

Aidha, alisema Rais Samia atakagua mradi wa bomba la mafuta pamoja na mradi mkubwa wa umwagiliaji wenye thamani ya sh. bilioni18.

Alisema kwenye ziara hiyo pamoja na miradi mingi atakayokagua na kuzindua, Rais Samia atazindua shule ya sekondari ya watoto wa kike ya masomo ya Sayansi. “Tuna miradi mingi ambayo Rais Samia atakagua na kuzindua.

Lakini atazungumza na wananchi kupitia mikutano ya njiani pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano mkubwa wa mkoa.”

Alisema kwa ziara hiyo ya Rais ana imani Uwanja ya Mkwakwani hautatosha. Aliwataka watu wote viongozi wote wajitokeze kumpokea Rais Samia .

Alitaka hamasa iwe kubwa kwa sababu mambo ambayo amefanya mkoani Tanga ni makubwa.