January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Mary Masanja wilayani Mkuranga

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Mkuranga alipofanya ziara leo, ambapo amewataka kubuni mbinu mpya za kuongeza idadi ya watalii katika eneo la misitu wanalomiliki.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiwa ameongozana na Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo kukagua eneo lililopandwa miche ya miti iliyo kwenye Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Mkuranga alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo.Wengine ni baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Mhifadhi wa Misitu Wilaya ya Mkuranga wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Charles Kaselya (kushoto) akitoa maelezo ya  utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb)(katikati) leo Wilaya ya Mkuranga. Kulia ni Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo
7
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mary Masanja (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi  ya watumishi wa  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Wilaya ya Mkuranga. Wengine ni Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof.Dos Santos Silayo (katikati) na Mhifadhi wa Misitu Wilaya ya Mkuranga Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Charles Kaselya (wa pili kulia).
Â