Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wakala wa Chakula na dawa Zanzibar (ZFDA) wamewataka wafanyabiashara kutokujaza bidhaa katika makontena na badala yake kuwacha nafasi ya kuweza kuruhusu hewa kuingia ili kuepusha kuharibika kwa bidhaa kunakosababishwa na joto.
Wito huo umetolewa na Afisa kutoka wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA)Mohammed Shauri wakati walipofika katika ghala la kampuni ya Sahal Geaneral Store liliopo Malindi kwa ajili ya ukaguzi na kugundua tani zaidi ya mia moja za Mchele zilizoingizwa kutoka Pakistan zimeharibika kwa kubadilika rangi na kuingia wadudu ,hivyo mchele huo umezuiliwa kwa matumizi ya Binaadamu.
Akielezea sababu zilizopelekea kuharibika kwamchele huo amesema ni pamoja na joto lililochangiwa na ujaaji wa Bidhaa hiyo na kukaa sana kwenye makontena kulikotokana na uzorotaji wa ufuataji wa taratibu za Bandari kwa Wafanya Biashara.
“Niwashauri Wafanya Biashara kufuata taratibu mapema ili kuepusha bidhaa zao kukaa muda mrefu ndani ya makontena kunakopelekea kuharibika kwa bidhaa hizo na kusababisha hasara kwao na madhara kwa jamii”. alishauri Afisa huyo.
Aidha amewaomba Wafanya biashara kuacha kuingiza bidhaa masokoni mara tu wanapoona dalili za kuharibika kwa bihaa hizo na badala yake kufika ZFDA kwa ajili ya ukaguzi ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.
Mapema Afisa kutoka ZFDA aliitaka kampuni ya Sahal General Store kufuata taratibu watakazopewa na ZFDA ili kuuteketeza Mchele huo kwani unaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa utoaji wa mizigo Bandarini katika kampuni ya Sahal General Store Juma Abubakar Alhaji amesema kuharibika kwa mchele huo kumechangiwa na joto lililosababishwa na ukaaji wa muda mrefu Bandarini ,hivyo ameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya Bandari ili kuepusha msongamano wa meli za makontena Bandarini kunakopelekea kuchelewa kushushwa kwa makontena.
Aidha bwana Juma amesema wapo tayari kushirikiana na Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar kuhakikisha mchele huo hautumiwi na binaadamu kwani wapo kwaajili ya kulinda Afya za Binaadamu na sio kuwaangamiza.
Ukaguzi wa ZFDA umefanyika kufuatia kampuni ya Sahal General Store kujisalimisha mara baada ya kuhisi mchele huo walioingiza haufai kwa matumizi ya Binaadamu .
Asante
More Stories
Serikali ya Kijiji Ilungu yawakatia bima za afya wananchi 1500
TMA kuendelea kufuatilia mifumo yake
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi