Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema Umefika Wakati kwa Zanzibar Kuzalisha Vipaji vya Vijana watakaokuwa na Uwezo wa kucheza Nje ya Nchi.
Rais Dk, Mwinyi ametoa tamko hilo alipoweka jiwe la Msingi la Ukarabati Mkubwa wa Uwanja wa Gombani na Viwanja vyengine Wilaya ya Chake Chake , Mkoa wa Kusini Pemba.
Dk,Mwinyi ameeleza kuwa hatua ya Kuvikarabati Viwanja vya New Amaan Complex, Mao Tse Tung na Gombani na Ujenzi wa Viwanja 17 kila Wilaya Unalenga kuibua Vipaji Nchi Nzima Katika Ngazi Zote
” Hatuwezi Kuibua Vipaji vya Vijana katika Maeneo ya Mjini pekee ni lazima twende hadi Vijijini kuibua Vipaji vilivyojificha”
Rais Dk, Mwinyi amesisitiza kuwa Ilani ya Uchaguzi ilieleza Kufanyika Ukarabati jwa Uwanja wa Amani pekee lakini Serikali imevuka Malengo kwa Viwanja vya Wilaya na Inalenga kujenga Academy kila Mkoa.
Dk,Mwinyi amefafanua kuwa Wachezaji Wakubwa wanaotamba katika ligi za Uingereza ,Hispania na Italia wametoka katika Academy za Soka katika nchi zao jambo alilolielezea kuwa ni lazima lifanyike Zanzibar.
Ameongeza kuwa Serikali inaweka Mkazo katika Ukarabati wa Uwanja wa New Amani Complex Utumike Ipasavyo katika Michuano ya CHAN itakayofanyika nchini Mwezi wa Februari mwaka Huu na Michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika Mwaka 2027 Tanzania Ikiwa Mwenyeji kwa kushirikiana na Uganda na Kenya.
Rais Dk, Mwinyi ametoa Agizo kwa wote wanaohusika kuhakikisha wanatoa Ushirikiano kwa Mkandarasi wa Uwanja wa Gombani REFORM SPORTS ili kukamilisha Ukarabati huo kwa wakati ili Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi yafanyike Uwanjani hapo.
Aidha Rais Dk, Mwinyi ameitakia kila heri Timu ya Taifa ya Zanzibar ZANZIBAR HEROES inayoshiriki Michuano ya Mapinduzi kufanya vema na Kushinda Kombe hilo.
Naye Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita amesema Wizara hiyo Imejipanga kusimamia vema Miradi yote ya Michezo kwa ajili ya kukamilika kwa Ufanisi zaidi.
Akizungumza Katika hafla hiyo Mkandaarasi Moussa Bey ameeleza kuwa Kuaminika Na Serikali na Kukabidhiwa kazi ya Ukarabati wa Uwanja wa Gombani ni Heshima ya Kipekee na kumuelezea Rais Mwinyi kuwa miongoni mwa Viongozi wa Mfano Barani Afrika anaependa Maendeleo
Uwanja wa Gombani Unafanyiwa Ukarabati Mkubwa ikiwemo Uwekaji wa paa jipya ,Ujenzi wa kuta ,Vyumba vya Wachezaji,Eneo la Watu Mashuhuri, Maegesho,Tartan ,Uwekaji wa Minara, Mifumo ya Maji na Umeme pamoja na Ujenzi wa Uwanja wa Mazoezi pembezoni mwa Uwanja huo.
Ukarabati huo wa Awamu ya Pili utagharimu kiasi cha Dola za Marekani Milioni 4,250,000 unafanywa na Kampuni ya REFORM SPORTS ya Uturuki.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango