Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipa nchi hiyo hekta 20 za ardhi kwa ajili ya kuhudumia mizigo ya nchi hiyo.
Rais Hichilema amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari alioufanya na Rais Samia kwenye Ikulu ya Zambia iliyopo jijini Lusaka.
Rais Hichilema alisema Wazambia wamechukua hatua hiyo kama zawadi ya kuonyesha ushirikiano mwema baina ya nchi hizi mbili.
Katika hotuba yake kama mgeni rasmi wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia yaliyofanyika jana jijini Lusaka, Rais Samia alisema eneo ambalo Zambia itapewa liko Kwala, mkoani Pwani.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto