April 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zaidi ya wananchi 500 Karume wapewa mkono wa Eid

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Karume wilayani Ilala jijini Dar,Hajji Bechina,ametoa chakula kwa ajili ya sikukuu ya Eid kwa wananchi 560 vyenye thamani ya milioni 10.

Akizungumza katika tukio hilo Bechina,amesema ametoa sadaka hiyo kwa wananchi na makundi maalum.Ambapo kila mwaka amekuwa alifanya hivyo

Sanjari na hayo alikabidhi runinga ya inchi 46 kwa vijiwe viwili vya Young Star na Wachonga vinyango vyote vya Ilala,huku akiwahimiza wananchi kuchagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi(CCM), katika uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwaka huu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ilala, Said Sidde,amewahimiza Wenyeviti na viongozi wengine kuiga mfano wa Mwenyekiti huyo wa kuwajali wananchi wake.