Na Prona Mumwi, timesmajira
Jumla ya Vijana 763 wahitimu wa awamu ya kwanza ya mafunzo ya programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Build a Better Tomorrow – BBT), wametembelea eneo la mashamba ya pamoja ‘block farm’ lililopo Mlazo, Ndogowe ambapo watapatiwa na Serikali mashamba na maeneo ya makazi.
Eneo hilo ambalo lipo kwenye hatua ya maandalizi ni moja ya maeneo ambayo Wahitimu hao watakabidhiwa ardhi na hati kila mmoja kwa muda wa miaka 66.
Mratibu wa programu ya BBT, Vumilia Zikankuba amebainisha kuwa katika eneo hilo la Ndogowe zimepatikana hekari takribani 11,453 ambazo hazijawai kutumika katika shughul za kilimo.
Aidha, Haruni Lucas Diwani wa Kata ya Mhambako, Mlazo ameipongeza Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo wa BBT na ameahidi kutoa ushirikiano unaotakiwa.
More Stories
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu
Jeshi la Polisi Katavi laanika mafanikio 2024