MILWAUKEE, Washington,
NYOTA wa kikapu katika timu ya Atlanta Hawks, Trae Young ameisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa vikapu 116-113 dhidi ya Milwaukee Bucks katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Ligi Kuu ya Kikapu nchini Marekani NBA, ukanda wa Mashariki uliofanyika usiku wa juzi.
Katika mchezo huo Young aliifungia timu yake alama 48, John Collins aliongeza alama 23 na marudio 15 huku Capela akiwa na alama 12 na marudio 19 kuhakikisha timu yao inaibuka na ushindi.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo nyota wa Atlanta Trae Young alisema, anafurahi kuisaidia timu yake kupata ushindi kwani mchezo wa mpira wa kikapu upo kwenye damu na siku zote anapenda kupata matokeo chanya.
Kwa upande wa Milwaukee Bucks nyota wa timu hiyo Giannis Antetokounmpo aliifungia timu yake alama 34, marudio 12 na asisti tisa huku Jrue ikiongeza alama 33 na misaada 10.
Hawks hawakuwahi kushinda mchezo wa fainali wa Mkutano wa Mashariki tangu kuhamia Atlanta mnamo 1968. Timu hiyo ilifika fainali za Mashariki mnamo 2015, lakini walifagiliwa na Cleveland.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania