January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Yemi Alade

Yemi Alade kuwakomboa wanawake kupitia UNDP

ABUJA, Nigeria

MWANAMUZIKI kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade amehaidi kutumia sauti yake kwa ajili ya kuwakomboa wanawake mara baada Umoja wa mataifa kumtangaza kuwa balozi wao.

Yemi, mwenye umri wa miaka 31 raia wa Nigeria ametajwa kuwa balozi wa nia njema na shirika la kimataifa la maendeleo (UNDP).

Akizungumzia hilo kupitia kwenye Video yake, Yemi amessema atawaangazia wale wanaoangaika kiuchumi na kijamii kutokana na athari za mlipuko wa corona.

Yemi amesema, yuko tayari kutoa suluhu ya changamoto nyingi kupitia ubunifu wake. Wanawake ni miongoni mwa watu bilioni 4 ambao wanajaribu kukabiliana na corona bila ya kupata usaidizi wowote.