Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KAMPUNI ya Mawasiliano hapa nchini, Yas imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga almaarufu Bombo Hospital kwa ajili ya huduma za afya.
Msaada huo ni sehemu ya mkakati wa Yas wa uwajibikaji kwa jamii (CSR), ukiwalenga kuboresha huduma za afya kwa wanawake na watoto wanaohudumiwa na hospitali hiyo ambayo hupokea zaidi ya wagonjwa 2,500 kila mwezi.
Lakini pia, vifaa hivyo vitasaidia kupunguza mzigo kwa wahudumu wa afya, na vitatoa nafasi kwa watanzania kupata huduma nzuri zaidi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo hivi karibuni, Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Pwani Kaskazini, Abdul Ally amesema wameamua kwenda katika Hospitali ya Bombo, kutokana na hospitali hiyo kuwa kitovu cha matibabu kwa Mkoa wa Tanga,lakini pia ni tumaini kwa maelfu ya watanzania.
“Sisi Yas, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha watanzania wanapata mawasiliano ya uhakika na kuwaunganisha na fursa mbalimbali za kidijitali lakini nje ya minara, na masuala ya teknolojia, tunaamini kwamba hakuna njia bora ya kuinganisha na jamii zaidi ya kuwapatia huduma zinazogusa maisha yao ya moja kwa moja hususan zikiwa ni huduma za afya.
“Hii ni hospitali inayohudumia zaidi ya watu 2,500 kwa mwezi huku asilimia kubwa wakiwa wanawake na watoto. Katika kutekeleza mkakati wetu wa Uwajibikaji kwa jamii (CSR), Yas tumeweka Afya kama moja ya vipaumbele vyetu vikuu.

“Tunafahamu kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, wanawake 5 kati ya 10 hapa nchini hupata changamoto wakati wa kujifungua kutokana na sababu mbalimbaliKwa kuzingatia changamoto hizi, tumeona ni vyema kuchangia kwa vitendo – na leo tunakabidhi vifaa mbalimbali katika Hospitali hii ya Bombo,” amesema Abdul Ally.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni, vitanda vya hospitali Magodoro na mashuka, vitanda maalum vya kujifungulia, vifaa vya kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto tumboni (fetal dopplers), vifaa vya kujifungulia salama (Maternity Kits) na Gumboots kwa watumishi wa afya.
Aidha, amesisitiza kuwa wao kama Yas wataendelea kuwa mshirika wa karibu wa maendeleo ya jamii kwa mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.

More Stories
Jiji la Dar-es-Salaam latenga bilioni 18 za mkopo wa asilimia 10Â
Aweso:Rais Samia ameweza kumtua mwanamke ndoo kichwani
Jukwaa la wanawake Ilala laadhimia kumuunga mkono Rais Samia