March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Yas yakabidhi zawadi kwa washindi droo ya pili

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

KAMPUNI ya mawasiliano Yas imekabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya pili ya Kampeni yake ya ‘Tunasheherekea Pamoja Mwaka Mmoja wa Yas.

Lengo ikiwa ni muendelezo wa juhudi za kampuni hiyo kuwashukuru na kusherehekea na wateja wake kwa kutimiza mwaka mmoja tangu kurejea sokoni.

Katika droo hiyo, washindi mbalimbali walijipatia zawadi ikiwemo fedha taslimu ambapo washindi saba walikabidhiwa Sh milioni moja kila mmoja.

Mshindi mmoja wa wiki alojinyakulia Sh milioni 5. Zawadi nyingine zilizotolewa ni simu janja saba na 5G routers saba.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam, hivi karibuni, Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa wa Yas, Ndevonaeli Eliakimu amesema kampeni hiyo inaendelea kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wateja.

Hali hiyo inathibitisha umuhimu wa kuenzi na kuimarisha uhusiano baina ya kampuni na watumiaji wake.

Ameeleza kuwa, kampeni hiyo ni sehemu ya dhamira ya Yas kuhakikisha Watanzania wanaendelea kunufaika na huduma za mawasiliano zilizo bora, nafuu na bunifu.

Eliakimu ameongeza kuwa, katika droo hiyo ya pili, kampuni imefanikiwa pia kupata washindi 10 wa safari ya Dubai, safari ambayo inatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Amesema, zawadi hizo zinazidi kuongeza hamasa kwa wateja kutumia huduma za Yas katika kipindi ambacho kampuni inaendelea kufanya uwekezaji katika kuboresha upatikanaji na ubora wa mtandao wake.

Miongoni mwa washindi ni Noela Kasinda, ambaye aliyeshinda Sh milioni 5.

Akiwashukuru Yas, Kasinda amesema ushindi huo umeleta matumaini mapya kwa familia yake na umedhihirisha dhamira ya kampuni hiyo kuthamini wateja wake.

Amesema, “Sikutegemea kabisa kushinda kiasi hiki. Nawashukuru sana Yas kwa kutambua thamani ya wateja wao. Ushindi huu umenipa nguvu ya kuendelea kutumia huduma za Yas kila siku,” alisema.

Kampeni ya ‘Tunasheherekea Pamoja Mwaka Mmoja wa Yas’ inaendelea kote nchini, na wateja wanaendelea kupata nafasi ya kuingia kwenye droo kupitia matumizi yao ya kawaida ya huduma za mawasiliano za Yas.

Ushawishi wa kushiriki bado ni mkubwa, na utaratibu wa kushiriki ni rahisi kwa kununua vifurushi au kutumia huduma yoyote ya Yas